TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 24 Novemba 2014

G5 MODERN TAARAB USO KWA USO NA TWANGA PEPETA, JE WAPI NA LINI?.

NA KAIS MUSSA KAIS

              Bendi ya G5 Modern Taarab yenye makazi yake mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar, inaendelea na program yake ya burudani kwa kufanya show ya nguvu na yakihistoria na bendi ya dansi ya Twanga pepeta katika ukumbi wa LEKAM ROYAL HOTEL uliopo maeneo ya buguruni siku ya Alhamisi ya tarehe 4/12/2014 kwa kiingilio cha shilingi elfu sita tu 6000/=.

            Kabla ya kukutana na Twanga Pepeta siku hiyo ya tarehe 4!, bendi hiyo imeandaa onyesho la kukata na shoka kwa wakazi wa msasani na vitongoji vyake kwa kufanya show katika ukumbi wa CC CLUB uliopo msasani siku ya ijumaa ya tarehe 28/11/2014 kwa kiingilio cha shilingi elfu tano tu 5000/=.
MWINJUMA MUUMIN WA G5 MODERN TAARAB.

          Tarehe 5/12/2014 ijumaa ya mwezi ujao bendi hii itakuwa maeneo ya kibiti katika ukumbi w KIBITI LIVE. akizungumza na mtandao huu, mkurugenzi wa G5 Modern Taarab Hamisi Slim alisema anatarajia kushusha kikosi chote katika show hizo na wapenzi wategemee kupata burudani ya nguvu sana.Katika show hiyo ya kibiti kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu saba tu 7000/=.

ASHURA MACHUPA WA G5 MODERN TAARAB.
          Bendi hii imekuwa ikifanya show katika ukumbi wa Flamingo Night Club magomeni kwa shekhe yahya, kila siku ya Jumamosi nyote mnakaribishwa. Na kwa sasa inajiandaa kufanya shooting ya nyimbo zake mpya pamoja na kuweka kambi kwa ajili ya uzinduzi unaotarajia kufanyika mwezi wa kumi na mbili lakini tarehe bado haijawekwa wazi na uongozi wa bendi hiyo.

.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni