Bendi yako uipendayo ya Dar Modern Taarab inatarajia kurudisha burudani rasmi katika ukumbi wake wa KOPAKABANA uliopo maeneo ya mwananyamala A jijini Dar. Bendi hiyo ambayo hapo kabla ilikuwa ikitowa burudani katika ukumbi huo kwa siku za Jumanne ilisimama kidogo ili kupisha maandalizi ya uzinduzi wa albam mbili kwa pamoja ambao umeshafanyika katika ukumbi wa travetine mwaka huu.
DAR MODERN TAARAB WAKIWA STEJI. |
Akizungumza na mtandao huu meneja wa bendi hiyo Mr Bakari aliwaomba wakazi wa mwananyamala na vitongoji vyake kuwapa sapoti kubwa kama walivyokuwa wakifanya hapo nyuma, hii ni bendi yao nasi tumeamua kurudi tena nyumbani baada ya kukaa nao mbali kwa muda alimalizia kwa kusema.
Dar Modern ni bendi bora kwa sasa, na ni miongoni mwa bendi ambazo zitashiriki tamasha la mitikisiko ya pwani mwaka huu hapa nchini tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni