Tamasha bora kabisa kwa sasa linaloshirikisha bendi mbalimbali za taarab toka katika ukanda wa afrika mashariki na kati linalokwenda kwa jina la COAST NIGHT ambalo kila mwaka hufanyika mara moja katika nchi ya kenya, mara hii limetangazwa tarehe mapema ili bendi ziweze kufanya maandalizi na kujipanga vyema tayari kwa kuwapa burudani iliyo sahihi wakazi wa nchi hizo.Tarehe hiyo ni 3/04/2015 siku ya ijumaa.
BENDI YA MASHAUZI CLASSIC, HAPA WAKIFANYA YAO KATIKA TAMASHA LA COAST NIGHT NAIROBI KENYA MWAKA JANA. |
Unajua sheria ya tamasha hili huwa haturudii bendi mara zaidi ya moja kwahiyo kila bendi ina uwezo wa kushiriki kulingana na ubora wa kazi yake, ninachowaasa viongozi wa bendi za taarabu wawe na maandalizi yaliyo kamili.
Tamasha hili limekuwa likijizolea umaarufu kila mwaka kutokana ubora wake na utaratibu bora wa kushiriki kwa bendi za nchi husika. Mtandao huu unatoa pongezi kubwa kwa waandaaji wa tamasha hili la Coast Night Nairobi Kenya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni