Jokha Kasim ni muimbaji mwenye kipaji kikubwa sana katika tasnia yetu ya Taarab nchini Tanzania, Jokha ni mke wa mkurugenzi wa T MOTTO Amin Salmin ambae kwa sasa anatamba na jisongi la Domo la Udaku. Nilipata nafasi ya kuzungumza na gwiji huyo akiwa nyumbani kwake.
JOKHA KASIM. |
T MOTTO MODERN TAARAB WAKIWA STEJI. |
Ndipo nilipomtupia swali la kizushi kwamba je kwa hivi sasa ni muimbaji gani ambae anamsumbua akilini mwake kila amsikiapo hewani?. kwanza alicheka sana alafu akajibu kiukweli sina ninae mhofia katika tasnia yetu hii ya taarabu, ila wao wanaposikia Jokha anakuja na kitu fulani basi wanaungulika mioyoni mwao. nawaambia wajipange sana kunipoteza, mimi ni mtu na bahati yangu mjini. Hayo ndio majigambo ya Jokha Kasim mamaa wa kithethe!!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni