Thabit Abdul ni director na mkurugenzi wa bendi ya wakaliwao modern taradance ya jijini Dar, Thabit ni bingwa wa kuibua vipaji vya waimbaji wengi wa taarab hapa nchini na wengine wana majina makubwa mpaka sasa. Wakati nipo mitamboni kuandaa stori nilipokea simu ya Jumanne Ulaya akilalamika kwamba Thabit Abdul amekuwa akimchafulia jina kwa tuhuma zisizo za kweli jambo ambalo linamuumiza sana.
THABIT ABDUL. |
Aliendelea kueleza kwamba amekuwa akishangazwa sana na maneno ya Director huyo anayoyasambaza kwa wasanii tofauti kwamba eti yeye Jumanne Ulaya ndio amemshawishi mpiga bess wake Shomari Zizzou ahame toka bendi ya Wakaliwao na kujiunga na Ogopa Kopa!, mimi kama Jumanne Ulaya nasema kwamba kilichomuondoa Shomari pale Wakaliwao ni njaa na sivinginevyo!, nimepigia sana Wakaliwao kuna njaa pale asikwambie mtu kaka!.
JUMANNE ULAYA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni