NA KAIS MUSSA KAIS
Siku ya ndoa yetu ilikuwa ni furaha iliyoje kuweza kufikia malengo yetu tuliyojiwekea, tulikuwa ni wenye sura za tabasamu na bashasha kubwa watu walikula na kusaza, nitaendelea kukukumbuka japo naumia sana Nyawana.
|
HAPO NYAWANA AKIHOJIWA NA GEAH HABIBU. |
Gea Habibu wa Clouds Fm alituletea gari lake tukapanda maharusi tukiwapungia mikono wapendwa wetu wakati tunaelekea Hotelini kupumzika, ama kweli kila nafsi itaonja umauti, Nyawana sijui nitumie maneno gani ili jamii ielewe ni kwa kiasi gani tulipendana, ila kikubwa pumzika kwa amani,
|
SIKU YA NDOA YETU, HAPO TUKIHOJIWA NA GEAH HABIBU WA CLOUD'S FM. |
Mwenyezimungu akupunguzie adhabu za kaburi na akupe kauli thabiti, pia akupe kitabu cha Quraan kwa mkono wa kulia inshallah!, uwe ni mwenye kheli nyawana, unakumbukwa na familia yako, wapenzi wa muziki wako, Baba yako mzee Isale, watoto wako wapendwa Saidi na Queen pamoja nami mumeo Kais Mussa Kais ambae nimekuwa nikikulilia kila kukicha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni