TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 10 Novemba 2014

HII NI HISTORIA FUPI YA MAREHEMU NYAWANA KAIS MUSSA KAIS!, NITAKUKUMBUKA DAIMA MILELE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.
NYAWANA KAIS MUSSA KAIS.
Marehemu Nyawana Fundikira alizaliwa mwaka 1977 katika hospitali ya Muhimbili iliyopo Dar es salaam, ilipofika tarehe 11-11-2013 ndio siku yake aliyoandikiwa kurudi kwa mola wake. Amezikwa kijijini kwao huko mkoani Tabora siku mbili baada ya kifo chake.
Marehemu enzi za uhai wake, alijipatia elimu yake ya msingi katika shule ya Zanaki baadae akajiunga na shule za Masjid Quba na Alharamyn kwa elimu yake ya sekondari. Baada ya hapo akaenda kusomea taaluma ya uandishi wa habari. Alipomaliza taaluma yake ya habari alitulia nyumbani kwao mkoani, Tabora. Katika mchakato wa kutafuta maisha alifanikiwa kushinda taji la Miss Tabora mwaka 1996 (MALKIA WA KINYAMWEZI),


 Kisha akawa mtangazaji maarufu wa radio iitwayo ya Voice Of Tabora."VOT"  Katika shughuli zake akajikita na masuala ya uimbaji wa taarabu. Kazi yake ya mwanzo ilikuwa inaitwa Niko kamili nimejipanga, wimbo uliyomtangaza vizuri kisha alienda akajiunga na kundi la King's Modern Taarab, hakukaa sana  akahamia katika bendi ya T MOTTO. Hapo alipata kurekodi wimbo uitwao "Behind the scene" nyuma ya pazia. Kutokana nakuwa na elimu ya uandishi wa habari pamoja na uimbaji, akabahatika kutangaza vipindi vya taarab katika radio PASSION FM ya jijini Dar es salaam.
Licha ya kuwa na T MOTTO pia alitowa nyimbo zake mwenyewe ziitwazo umesharoga wangapi, Harusi ya mwanangu na shetani kataja jina.



NYAWANA KAIS MUSSA KAIS.

 Ameacha Mume anaefahamika kwa jina la KAIS MUSSA KAIS pamoja na watoto wawili Said na Queen aliyezaa na mume wake wa mwanzo huko Tabora.
Marehemu alitoa mchango mkubwa katika kuutangaza muziki wa taarabu na kuna habari kwamba eti
marehemu alijitabiria kifo katika wimbo wake wa shetani kataja jina wimbo huo alimuimbia mumewe, katika kutia vionjo alitumia lugha ya Kiingereza yenye maana "Kais... ni mtu wake wa mwisho katika dunia" Hii ni mistari ya wimbo huo alomuimbia Mumewe!.
"Kweli nimeamini,
kila jini na fundi wake,
kwa huyu bwana sisemi,
ndio chaguo lake,
nampikia maini,
anajiramba kwa raha zake,
jini wake subiani,
mimi ndio chano chake,
nampa mambo fulani,
kuniganda haki yake,
fundi yake ni mimi,
namkidhi haja za

 MWENYEZIMUNGU AKUPE KAULI THABIT MKE WANGU, INSHALLAH!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni