Leo ni siku ya hudhuni kubwa sana kwangu kwani ni siku uliyoiaga dunia na kuniacha peke yangu Nyawana, nikiikumbuka ilivyokuwa naumia nafsi na kubaki na majonzi moyoni. Nyawana tulipendana sana hakuna asiejua hilo, ulikuwa kama pacha wangu hata kama unaenda redioni kutangaza kipindi chako hukubali kurudi nyumbani peke yako mpaka nikufuate mke wangu, kila tulipokwenda ulikuwa ubavuni mwangu Nakumbuka siku ya kwanza kabisa kukutana na wewe mke wangu, ulikuwa umevaa kiheshima umetulia sehemu, nilikufuata na kukusalimu kwavile nilishawahi kukuona ktk televisheni ukifanya mahojiano na Sakina Lyoka wa Clouds, nilijitambulisha ukanielewa na kuanza mazungumzo yetu.
NYAWANA KAIS MUSSA, HAPA ALIKUWA NA UJAUZITO WA MIEZI MIWILI LAKINI ULITOKA KWA BAHATI MBAYA. |
Naikumbuka siku tupo kitandani ulinitamkia, mume wangu kwakuwa nakupenda sana basi naomba nikutungie wimbo wa kukusifia kabla sijakufa! nilishangazwa sana na kauli yako, lakini wewe ulisisitiza ndipo ulipochukuwa karamu na karatasi ukanitungia ule wimbo wa SHETANI KATAJA JINA. Roho inaniuma sana, kwanini uliniacha nyawana, kila nikifikilia naona kama vile ulikiona kifo kikikusogelea sema ulishindwa kuniambia ukihofu utaniumiza sana mke wangu. Tumefanya mengi ya mapenzi dear!.
NYWANA KAIS MUSSA AKIWA MWENYE FURAHA. |
Siku unafariki dunia ulinitamkia maneno ambayo mpaka sasa yanajirudia sana moyoni mwangu uliniambia "Kais mume wangu, mimi nakufa huku nakupenda sana, sidhani kama nilishawahi kumpenda mwanaume kama ninavyokupenda wewe!, wewe ndio chaguo langu sahihi lakini nasikitika nakuacha peke yako". Roho inaniuma sipendi kuyakumbuka maneno yale sana mke wangu. Tulisafirisha msiba na kwenda kukuzika Tabora siku ya tarehe 13/11 Nyawana mke wangu, naahidi nitakuja TENA KATIKA KABURI LAKO NYAWANA WANGU. mwenyezimungu namuomba akupunguzie madhambi yako, akuondoshee adhabu za kaburi na pia akupe kivuli miongoni mwa vivuli vya peponi mke wangu, nakupenda sana Nyawana.
NYAWANA KAIS MUSSA KAIS, PUMZIKA KWA AMANI MKE WANGU KIPENZI. |
Nilipooa tena baada ya wewe kufariki, maneno mengi yaliongewa kwamba sikupendi ndio sababu nimeoa, lakini ukweli nakupenda sana nyawana imenilazimu kuoa tena sababu mimi ni mtoto wa kiislam na najua maadili siwezi kukufanyia Dua nzuri kama nitakuwa naendelea kuzini Nyawana wangu, huyu mke wangu wa sasa AISHA ZAHIL ALLY ZORRO ni muelewa na amekuwa mstari wa mbele kuniambia tukufanyie Dua mke wangu, na taratibu zetu kila alhamisi ni lazima tufanye kisomo kwa ajili yako nyawana mke wangu. Nakili kusema wazi nakupenda sana nyawana wangu, nipo sawa na watoto wetu wote wapenzi Saidi Nyawana na Queen!. MUNGU AKUPUMZISHE KWA AMANI NYAWANA WANGU, LEO NITAKUFANYIA KISOMO HAPA NYUMBANI, ILI MWENYEZIMUNGU AKUPUNGUZIE MADHAMBI INSHALLAH!.PUMZIKA KWA AMANI MKE WANGU!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni