TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 30 Novemba 2014

MISAMBANO AANDAA MIKAKATI YA KUWASHITAKI WOTE WANAOIMBA NYIMBO ZAKE PASIPO RUKSA YAKE!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                Hati miliki kwa wasanii wa fani mbalimbali ni muhimu sana kwa sasa kipindi ambacho soko la sanaa limeingiliwa na kupelekea wasanii kuibiwa kazi zao kila kukicha, tumekuwa tukishuhudia wasanii wa bongo fleva na Bongo movie wakikamata kazi zao ambazo wajanja wamekuwa wakizidurufu pasipo wenyewe kujua wala kufaidika kwa chochote kile.

ABDUL MISAMBANO.
        Abdul Misambano yeye ameamua kujitoa muhanga na kutangaza vita kwa yeyote yule ambae kwa namna moja ama ingine atakuwa anajinufaisha kupitia nyimbo zake ambazo tayari ameziimba na zinafanya vizuri katika media mbalimbali hapa nchini na nchi za jirani. Nimeshaenda COSOTA na tayari nimesajiri kazi zangu zote kihalali kabisa hivyo nitamchukulia hatua yeyote anaejinufaisha kupitia nyimbo zangu, kuanzia zile bendi zinazopiga nyimbo zangu kwenye ma-bar mpaka wale wanaouza kazi zangu feki.

       Kwa wale wanaopiga nyimbo zangu katika maharusi sitokuwa na tatizo nao, kwani mara nyingi mashabiki zangu huwa wanaomba sana wapigiwe ili watunzane. Naomba ieleweke sintokuwa na lawama na yeyote sababu nimeweka wazi msimamo wangu juu ya nyimbo zangu mwenyewe alimaliza kwa kusema.

    Misambano ameamua na tunaamini ataweza sababu amefuata taratibu za kisheria katika kulikataza jambo hili kwa wazi wazi kabisa, COSOTA ndio suruhisho kwa wasanii wote kuibiwa kazi zao, hebu amkeni nanyi mkasajiri kazi zenu na muweze kupata haki zenu stahiki, Hongera sana Abdul Misambano kwa kuliona hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni