TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 1 Desemba 2014

HISTORIA YA MUIMBAJI NGULI ZUHURA SHABBAN KATIKA MUZIKI WA TAARABU!.

NA KAIS MUSSA KAIS


MSOME BI ZUHURA SHAABAN HAPA.
MWIMBAJI WA TAARAB ALIYEFAHAMIKA KATIKA TATHNIA HII MWANZONI MWA 1990's.

HIVI SASA HAKUNA TAARAB KUNA MASHAKA TU YA MIDUMANGE - ZUHURA SHAABAN.
 
Hivi unamjua mwimbaji mkongwe wa taarab, Bi Zuhura Shaaban?
Zuhura Shaaban ni mwimbaji mkongwe kwa sasa katika tathnia ya taarab, tathnia hiyo aliianza mwaka 1992 kwa kuanza kuimba tarabu asilia.
Safari yake ya muziki aliianza nchini Oman baada ya kushinikizwa na mumewe kwa kuonekana ana muelekeo wa kuimba. Kabla ya hapo Bi Zuhura hakupenda kazi ya muziki japokuwa mama yake alikuwa ni muimbaji mzuri wa taarab asilia.
Kutumbukizwa katika muziki na mumewe kutoka Zanzibar hadi Oman na kuanza shughuli hiyo bendi yake ya mwanzo iitwayo LEO BAND. Baada ya hapo wakaenda Dubai yeye na mumewe ambako ndiko Melody walipoianzisha.
Ndani ya kundi la Melody alidumu nalo kwa kipindi cha miaka tisa (9), ambalo baada ya Dubai likaja Zanzibar na sasa lipo Dar es Salaam, Tanzania.
Baada ya hapo alijiunga na Zanzibar Stars ambako alidumu kwa kipindi cha miaka mitatu na baadae alienda bendi inayosemekana ni chimbuko la Zanzibar Stars ambayo ni New Zanzibar. Bendi yake ya mwisho ni Zanzibar One ambayo mpaka sasa ndipo alipo japokuwa yeye kwa sasa ameicha kutokana shughuli zake za biashara zinazoambatana na safari ya kwenda Dubai kwa kuikuza biashara yake.
 
TOFAUTI KATI YA TAARAB YA 1990's na SASA.
Bi Zuhura Shaaban ameishangaa sana taarab ya sasa kuwa ni ya mdumange, kunukishana majasho, mchiriku yaani haiyeleweki haieleweki ni vurugu mechi tu japokuwa yeye ameimba hiyo Modern (mipasho) lakini sasa imezidi balaa. Taarab ya zamani muimbaji unaimba unatulia jukwaani bila bugudha, na watazamaji wanatulia kwenye viti au hucheza taratibu bila kugasi wengine.
Pia anasema taarab ya sasa msanii wala hajafikisha albamu mbili tayari anajipa jina, wasanii wanajipa majina ovyo bila hata kupewa na wanaoijua taarab na wanataarab. Mtu atatoa nyimbo moja tu tayari anajipa jina, amesema wasanii wasijipe majina wasubiri kupewa.
 
WALIYOMGUSA KUIPENDA TAARAB, Ni waimbaji Moh'd Ilias, Abdalla Issa, Abdul-aziz, Rukia Ramadhan na Fatma Issa.
Bi Zuhura Shaaban baadhi ya nyimbo alizoimba ni Cheo Changu, Siadhiriki (EAST A MELODY), majaliwa yalivyo, sichagui sibagui, hasara zao pamoja na wimbo wa kama ni rahisi aliyouimbia Zanzibar One.
Pata shairi la moja wa nyimbo zake ambayo inang'ara mpaka hivi sasa ikichezwa iitwayo Siadhiriki.
"Mlitaka niadhirike,
kusudi lenu mucheke,
lakini Mola manani,
kanistiri mja wake,
sijui yalianzaje,
binadamu mumezoea hasama,
hata nifanyeje,
binadamu hatutendeleani mema."
Ha

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni