TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 1 Desemba 2014

PATRICIA HILLARY, MWANA DADA ALIETIKISA KATIKA MUZIKI WA TAARABU!.


 NA KAIS MUSSA KAIS

PATRICIA HILLARY AKIFANYA VITU VYAKE.
Miongoni mwa nyimbo zenye mahadhi ya mwambao zilizotokea kupendwa sanamiaka ya karibuni ni kama ule uliojulikana kama “Njiwa” uliokuwa na mashairi yenye maneno kama “ewe njiwa,ewe njiwa,peleka salamu”. Mwimbaji wa wimbo huo alikuwa ni Patricia Hillary, malkia wa taarabu enzi hizo. Pichani ni Patricia Hillary akifanya vitu vyake. Patricia bado anajishughulisha na muziki nakuna baadhi ya vibao vyake vya zamani amuvirudia upya katika style ya kisasa zaidi.

        Patricia yupo kimya sana sasa hivi, lakini wapenzi na mashabiki wake wamekuwa hawaishi kumuulizia na kutaka kujua taarifa zake anafanya nini katika kuendeleza muziki wake?. Ubuyuwataarabutz.blogspot.com unamshauri msanii huyu kutokaa kimya sana kiasi hiki na ikiwezekana atoe japo wimbo mmoja ili wapenzi wake wapate radha adimu ya sauti yake ambayo wamekuwa wakiikosa kwa kipindi kirefu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni