Kundi la SINA CHUKI, chini ya sauti ya zege Makame Faki, ni kundi bora kwa sasa afrika mashariki kwa mtindo wao wa kidumbaki
Wakiwa
wanazikata nyonga zao kwa taratibu na kwa namna ambavyo utafurahi ukiwatazama, Makame Faki utampenda sana akikuimbia PAJERO LINANISUMBUA huku sauti yake nzito ikiwa ni kinogesho tosha masikioni mwako.
Muziki
huu ambao uko karibu sana na taarabu unapagawisha zaidi kwa staili yake huru
ya mashairi na hasa miondoko katika maungo ambapo wengi wa watazamaji
wamekuwa wakilazimika kuvamia jukwaa na wengine wakihangaika.
DUMBAKI STYLE ambayo inatokana na fidla, sanduku, manyanga kama cherewa na ngoma
mbili ni muziki ambao unafanyiwa kazi zaidi katika maharusi kutokana na
ghani zake kugusa zaidi hisia za mapenzi.
Kuna nyimbo nyingi za kuelimisha ambazo zinaashilia raha ya mapenzi, shida za maisha na karaha za wajivuni.
Hebu tazama mwenyewe kidumbaki kilivyo utapenda!.
MAKAME FAKI AKITUMBUIZA |
WAPIGAJI WA VYOMBO VYA KIDUMBAKI WAKIWA STEJI |
WANENGUAJI WA MAKAME FAKI WAKISEREBUKA. |
HAPANA CHEZEA KIUNO CHA KIDUMBAKI WEWEE!. |
HAPA MAKAME FAKI NGOMA IMENOGA!. |
SHABIKI AKISHINDANA NA WACHEZA SHOW KUONYESHA UMAHILI, NAMNA YA UCHEZAJI WA NGOMA HIYO!. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni