TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 25 Desemba 2014

HII NI MPYA KABISA:- KAIS MUSSA KAIS, NI MENEJA MPYA WA GUSAGUSA MIN BENDI

NA MWANDISHI WETU.

             Mkurugenzi wa mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Kais Mussa Kais au ukipenda unaweza kumuita "mzee wa fitina mjini" amejiunga na bendi ya Gusagusa yenye maskani yake magomeni jijini Dar katika nafasi yake ile ile ya umeneja.

          Akizungumza na mtandao huu Kais alisema kwamba ameamua kuhamia Gusagusa Min Bendi ili kupata uzoefu zaidi kwani anaamini ana safari ndefu sana katika muziki huu na mafanikio hayawezi kuja pasipo kujituma zaidi, Nilipokuwa meneja wa Supershine Modern Taarab, nilijitahidi kufanya mambo makubwa sana, ikiwemo kuifanya bendi hiyo kuwa miongoni mwa bendi tano bora kwa mwaka 2013-2014 na kuingia katika tamasha la mitikisiko ya pwani.

KAIS MUSSA KAIS MENEJA MPYA WA GUSAGUSA MIN BENDI.
       Vile vile nimefanikiwa kufanya video ya albam "huna style" ambayo kwa sasa inaonyeshwa sana katika vituo mbalimbali vya televisheni nchini, nyimbo zao pia zimekuwa zikichezwa sana redioni mara kwa mara na hii inanifanya kutembea kifua mbele huku nikijivunia baadhi tu ya mafanikio ambayo nimeyawezesha pale Supershine Modern Taarab.

      Naomba ieleweke sina tatizo na kiongozi wala msanii yeyote katika bendi ya Supershine Modern Taarab na ndio maana hata wakati nataka kuondoka pale sikuondoka kienyeji, nilienda kuwaaga viongozi wenzangu pamoja na wasanii kwa ujumla na kikao maalum cha kuagana kilifanyika pale pale club baada tu ya kumalizika mazoezi. Nashukuru nao walinipa baraka zao na kunitakia kazi njema huko niendako, kwa sasa mimi ni meneja wa Gusagusa Min Bendi Chini ya mwana mama wa haja kabisa BI AFUA SULEIMAN, MZEE SULTAN NA SABAHAH SALUM MUCHACHO hawa ndio wasanii waandamizi japo BI MWANAHAWA ALLY nae yupo yupo kwa mbaaali! alimalizia kusema meneja huyo mpya Kais Mussa Kais.

KAIS MUSSA KAIS, MENEJA WA GUSAGUSA MIN BENDI NA MMILIKI WA BLOG HII.
      Sisi dawati zima la habari la mtandao huu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Tunapenda kumtakia mafanikio mema huko aendako sasa Bosi wetu, na tunamuomba mwenyezimungu amuwezeshe kufanya makubwa zaidi akiwa na Gusagusa ili kupandisha zaidi na zaidi C.V. yake katika kuongoza bendi mbalimbali za taarab hapa nchini tanzania, ikumbukwe kwamba Kais Mussa Kais ameshaongoza bendi zaidi ya tatu akiwa kama meneja, ya kwanza ni T MOTTO, ya pili ni KING'S na ya tatu ni SUPERSHINE na kwa muda huu ndio amekamata usukani katika kuifikisha pazuri GUSAGUSA MIN BEND.....mungu akubaliki sana Bosi wetu!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni