Kama wewe ni mdau haswa wa muziki wetu huu wa taarab hapa nchini basi ni wazi utakuwa unamfahamu mkongwe wa siku nyingi na mkung'utaji wa gitaa la sollo asie na mpinzani Mr Abdallah Bwigabwiga, ambae kwa sasa anapatikana katika bendi ya Supershine Modern Taarab yenye maskani yake magomeni jijini Dar, yeye ni kiongozi wa muziki katika bendi hiyo.
Bwigabwiga anasema Taarab ya sasa vijana wameibadilisha kabisa imekuwa si taarab haswa kama ile waliyokuwa wakiipiga wao enzi ya zanzibar stars, hebu jaribu kuchukuwa nyimbo za zanzibar stars za enzi hizo ambazo tumetengeneza sisi mfano "KAMA WEMA" ambao mimi ndio nimepiga Sollo, alafu uzilinganishe ni hizi za taradance kama wanavyozinadi wenyewe utaona kuna utofauti mkubwa sana kuanzia utunzi wa mashairi mpaka upangaji muziki, zetu japo ni za zamani lakini zina ubora mpaka leo.
ABDALLAH BWIGABWIGA AKIFANYA VITU VYAKE!. |
Soko la muziki wetu wa taarab linazidi kushuka, tusijidanganye kwamba soko lipo juu sikweli!, huwezi kulinganisha na zamani, taarab ya sasa inachanganywa na mnanda humo humo! hii ni ajabu sana kwakweli!. nawaomba madirector wenzangu tugeuke nyuma na tukumbuke wapi tumetoka na je huko tuendako au tunapoupeleka muziki huu kuna manufaa yoyote?...TUBADILIKE NI USHAURI TU!!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni