Mkurugenzi wa Coast Modern Taarab Omary Tego ameuthibitishia mtandao huu kwamba ni kweli ameamua kuongeza nguvu katika kikosi chake kwa kumchukuwa Shabban Kinanda toka Dar Modern Taarab, na yupo katika mipango nae na atarekodi katika albam hii ijayo.
Unajua nilibakiwa na mpigaji kinanda mmoja tu ambae ni mdogo wangu Yusuph Tego kwahiyo sasa hivi watakuwa wawili akishirikiana na Shabban Kinanda. "nimeplan" wote wawili kila mmoja atarekodi nyimbo tatu tatu na albam itakuwa na nyimbo sita.
Mtandao huu uliamua kumtafuta meneja wa Dar Modern Taarab Mr Bakary ili nae athibitishe je ni kweli Shabban Kinanda amehama katika bendi yake ama ni uzushi tu wa mitaani?. Yeye kwa upande wake alisema kwamba ni kweli Shabban Kinanda hayupo katika bendi yake na taarifa anazozisikia ni kwamba yupo Coast Modern Taarab, sina tatizo nae anaweza kwenda bendi yoyote ile sababu sikuwa na mkataba nae.
OMARY TEGO- MKURUGENZI WA COAST MODERN TAARAB. |
Aliendelea kwa kusema msanii yeyote anaejisikia anataka kuondoka na anajijua hana mkataba nasi basi ruhsa haina shida, ila kama tuna mkataba nae basi i
tabidi tukae chini ili tuangalie vifungu vya mkataba huo vinasemaje kuhusu yeye kuondoka bendi. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hapa Dar Modern alimazia kwa kusema.
Kama ambavyo tuliwaahidi wasomaji wetu kwamba tutawaletea muendelezo wa habari hii ili kupata ukweli halisi, natumaini mmeweza kuelewa vyema, na maelezo ya viongozi hao wote wawili yamejitosheleza kabisa, huu ndio mtandao makini ambao haubahatishi siku zote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni