TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 12 Januari 2015

BI AFUA SULEIMAN:- NILIISAMBARATISHA ZANZIBAR STAR'S DIAMOND JUBILEE NA KUPEWA JINA LA "B 52".

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Bi Afua Suleimani ni muimbaji wa muda mrefu sana katika tasnia hii ya taarabu nchini tanzania, mama yetu huyu ambae ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora ameitumikia bendi ya East African Melody kwa takribani miaka kumi.

          Nilianza mazungumzo na Bibi huyu kwa kumuuliza nini chimbuko la jina "B 52?" maana limechukuwa nafasi kubwa sana katika harakati zako za muziki huu hapa nchini!, Huku akicheka alianza kwa kusema unanikumbusha mbali sana kiukweli, ni historia ndefu ila nitaifupisha ili wapenzi wangu wapate kuelewa.

BI AFUA SULEIMAN AKIFANYA YAKE!.
        Wakati huo wimbo wa "Utalijua Jiji" unatamba kupita kiasi uliandaliwa mpambano kati ya East African Melody na Zanzibar Star's Modern Taarab katika ukumbi wa Diamond Jubilee, siku hiyo sitoisahau katika maisha yangu ya muiziki, watu walikuwa wengi sana na Zanzibar Star's ilikuwa inatamba mno!.

        Ziliimbwa nyimbo nyingi lakini niliponyanyuka mimi na kuimba Utalijua Jiji hapo ndipo nilipoisambaratisha kabisa! kabisa! bendi ya Zanzibar Star's, watu walipagawa kwa vifijo na mayowe ukumbi mzima hakuna alieweza kukaa kitini!, watu wote wakawa wanaimba kunifuata mimi!. Baada ya kumaliza kuimba nilikaa pembeni nikaanza kulia sana tena sana!, nililia kwa furaha kwani sikuwa nategemea kama naweza kuyafanya niliyoyafanya.

BI AFUA SULEIMAN AKIIMBA.
        Baada ya kupita kama wiki moja East African Melody tukazindua albam ya Utalijua Jiji katika ukumbi wa travetine magomeni, hapo ndipo lilipozaliwa jina la "B 52", Na alienipa jina hili ni mtangazaji "Masoud Masoud" kipindi hicho yupo redio tanzania. nakumbuka alisema sasa namkaribisha jukwaani Afua Suleiman "B 52" na kuanzia leo hili ndilo jina lake kwani aliisambaratisha Zanzibar Star's pale Diamond Jubilee! watu wakalipokea vyema na mpaka sasa natamba kwa jina hilo.

        Huyo ndio Bi Afua Suleiman "B 52" kwa sasa ni muimbaji wa bendi ya gusagusa min bend iliyo na maskani yake magomeni jijini Dar, mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unamtakia mafanikio zaidi katika maendeleo ya muziki wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni