NA KAIS MUSSA KAIS.
Mkurugenzi wa bendi ya Coast Modern Taarab, Omary Tego "The special one" amevunja ukimya kwa kusema kwamba kwa jinsi alivyojipanga anaamini wazi kabisa kwamba mwaka huu 2015 ni mwaka wa mafanikio kwa bendi yake ya Coast Modern Taarab.
|
OMARY TEGO NDANI YA VIDEO YA SURPRISE. |
Aliyasema hayo wakati akihojiwa na mtandao huu kuhusu malengo yake kimuziki hususani katika mwaka huu mpya wa 2015. Ndugu mwandishi kiukweli Taarab ya sasa haitaki papara inatakiwa utulie na ufanye jambo litakalo kuweka kwenye ramani kwa kipindi kirefu zaidi, Coast nimepanga kuanza na Maua Tego na wimbo wake mpya kabisa uitwao Mume ni bonge la Issue, baada ya hapo kuna chipukizi nitawatoa kama ujuavyo bendi hii kila mwaka ni lazima nitoe underground mmoja na baadae anakuja kuwa muimbaji mzuri zaidi.
|
OMARY TEGO AKIFANYA YAKE KWA MASHABIKI. |
Baada ya hapo ndipo nami kabali yao nitakuja na kitu changu kipya kabisa kwani watu wamekuwa wakinipigia sana simu kunisisitiza nitoe wimbo mwingine. alipoulizwa jina la wimbo ambao anatarajia kuimba yeye utaitwa kwa jina gani, alisema ni mapema mno na kwa sasa nisingependa kutaja kwani wajanja wamekaa masikio waluu! wakisikia Tittle ya wimbo tu! basi kesho utasikia kwenye bendi ingine, wasubiri tu kila jambo linahitaji subira.
Huyo ndio Omary Tego mkurugenzi wa bendi ya Coast Modern Taarab, bendi yenye maskani yake mtoni mtongani jijini Dar, bendi hii imekuwa ikifanya vizuri khali inayopelekea kupata show nyingi sana mikoani na hata nchi jirani ya kenya. Tusubiri ujio mpya ndani ya mwaka huu wa 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni