NA KAIS MUSSA KAIS.
Unapozungumzia wapiga ala za muziki hususani taarab hapa nchini basi katika gitaa la besi kwa sasa ni lazima utalitaja jina la Shomary Zizzou mpigaji wa Ogopa Kopa Classic Bendi.
|
SHOMARI ZIZZOU AKIWA NDANI YA UNIFORM ZA OGOPA KOPA CLASSIC. |
Shomary ameanzia mbali muziki huu lakini jina lake limekuja kuwika zaidi pale alipokuwa muajiliwa wa bendi ya Jahazi Modern Taarab kipindi hicho wakiwa sambamba na swahiba wake ambae kwa sasa ni marehemu aitwae Juma Mgunda. Lakini kwa bahati mbaya Jahazi ilipunguza wasanii na yeye pamoja na swahiba wake huyo walipunguzwa.
Hakukata tamaa kwani aliendelea kupambana kwenye muziki na kuelekea five stars modern taarab kipindi hicho inamilikiwa na mkubwa "Shark's the Don", hapo alikaa kwa muda mchache kabla Shark's mwenyewe kuamua kufungia vyombo vyake baada ya kukosana na uongozi na safari ya five star's ikaishia hapo.
|
SHOMARI ZIZZOU AKIWAJIBIKA. |
Alipotoka five star's alikaa kwa muda akitafakali nini afanye ndipo alipochukuliwa na Thabit Abdul mkombozi na kujiunga na bendi ya Wakaliwao ijapokuwa hakuwa na mkataba, pale alikuwa na Jumanne Ulaya kama ilivyokuwa wakati yupo five star's. Ilipoanzishwa Ogopa Kopa Classic Bendi, wa kwanza kuelekea kule alikuwa ni Jumanne Ulaya na kumuacha Zizzou akiwa bado anaendelea kuitumikia Wakaliwao, lakini ghafla Zizzou nae akaelekea Ogopa Kopa jambo lililopelekea mkurugenzi wa Wakaliwao kumtuhumu Jumanne Ulaya kwamba ndie alie mshawishi Zizzou kuitosa bendi yake na kwenda Ogopa Kopa.
|
SHOMARI ZIZZOU- MWANAUME KAZINI. |
Mtandao huu ulipata bahati ya kuzungumza na Shomary Zizzou na kutaka kujua baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakiwaumiza watu wanaomfahamu Ostaadh Zizzou au ukipenda muite mzee wa swala tano! kwani hakuna kipindi cha swala ambacho kinampita. kwanza tulitaka kujua ni kitu gani kilimfanya aondoke Wakaliwao wakati akijua wazi kwamba yeye ni mpigaji peke wa gitaa la besi aliebakia katika bendi hiyo?
Nae alijibu, Mimi nilifuatwa na viongozi wa bendi ya Ogopa Kopa wakiniomba kujiunga nao, nami baada ya kutimiziwa nilichokuwa nahitaji basi ndipo nilijiunga nao, hapa ukiangalia kikubwa ni maslahi na kubadili upepo tu lakini sina tatizo na Thabit Abdul. Swali la pili kwa sasa ni mpigaji gani wa gitaa la besi ambae unamhofia kwa uwezo wake?. Kiukweli hakuna, mimi najiamini na naweza kusema sina mpinzani kwa sasa wote ni watoto tu kwangu, labda wamenizidi kwa majina lakini sio uwezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni