Abdul Misambano ni mwanamuziki wa muda mrefu katika tasnia hii ya taarab hapa nchini tanzania, tokea akiwa burundi akifanya muziki huu mpaka alipoamua kurudi nyumbani tanzania na kujiunga na bendi ya Babloom alikuwa ni moto wa kuotea mbali haswa pale alipotoa wimbo wa "ASSU" ambao ulimtangaza sana na kumuweka juu katika ramani ya muziki huu hapa nchini mwetu.
Misambano kwa sasa ni muimbaji wa bendi ya TOT kwani pale ndio sehemu ya ajira yake halisi, ila amekuwa akionekana katika baadhi ya bendi ikiwemo Wakaliwao na G5 Modern Taarab akiimba na mpaka kufikia kurekodi wimbo mpya kabisa uitwao "SIO MIE NI MOYO" akiwa na bendi ya G5 Modern Taarab. Chakustaajabisha kila mahojiano anayofanya Misambano na baadhi ya vyombo vya habari T.V na REDIO amekuwa akisema kwamba wimbo wake wa sio mie ni moyo sio mali ya bendi ya G5 ingawa mkurugenzi wa bendi hiyo amegharamia kila kitu kuanzia mazoezini mpaka gharama za kurekodi studio!, Jambo hili lilinifanya kumtafuta misambano na kufanya nae mahojiano kama ifuatavyo:-
ABDUL MISAMBANO. |
UBUYU WA TAARAB:- Misambano kwanza kabisa heshima yako kiongozi, then twende kwenye point husika, nimekuwa nikikusikia ukizungumza katika MEDIA mbalimbali kwamba wimbo wa Sio mie ni Moyo ni mali yako na wala sio wa G5 je kuna ukweli wowote kaka juu ya jambo hili?.
MISAMBANO:- Ni kweli wimbo wa "SIO MIE NI MOYO" ni mali yangu mimi mwenyewe na wala hauhusiani kabisa na bendi ya G5 Modern Taarab ukweli ndio huo!.
UBUYU WA TAARAB:- Kivipi unasema wimbo hauhusiani kabisa na G5 wakati umefanya mazoezi na wasanii wa bendi hiyo na hata pesa za kulipia studio kurekodi zimetolewa na mkurugenzi Hamisi Slim? hebu fafanua!.
MISAMBANO:- Kulingana na makubaliano yangu mimi na Hamisi Slim ni kwamba mimi nifanye mazoezi na bendi yake then nikisharekodi kwa gharama zake ndipo tukae chini tuzungumze nimuuzie huu wimbo kiasi gani, lakini mpaka sasa naweza kusema amekiuka makubaliano yetu tuliyoafikiana na sipo tayari kumuuzia tena na sitaki kusikia wimbo wangu ukipigwa na G5 na sitaki chochote tu na wao!.
HAWA NI BAADHI YA WASANII WA G5 MODERN TAARAB. |
MISAMBANO:- Nimekwambia yeye ndio amekiuka makubaliano yetu kwahiyo asitegemee kama nitamrudishia hizo laki nne zake, kwanza bendi yake nimeitumikia sana tu, kwahiyo habari ndio hiyo na mpaka sasa nimeshaingia mkataba na kampuni ingine kwa ajili ya kufanya video nyimbo yangu hiyo ya SIO MIE NI MOYO ila ni mapema mno kuitaja kwa sasa.
Ubuyuwataarabutz.blogspot.com hatukuishia hapo tulimtafuta mkurugenzi wa bendi ya G5 Hamisi Slim ili nae azungumze kwa upande wake juu ya sakata hili nae alikuwa na haya yakusema:-
HAMISI SLIM:- Mimi mkurugenzi wa G5 Hamisi Slim nasema Abdul Misambano ni kweli nilimpokea tukawa na project ya kutengeneza nyimbo yake hiyo na kweli kwa gharama zangu tulifanikiwa kurekodi na kuipeleka nyimbo mpaka katika MEDIA mbalimbali na makubaliano yetu ilikuwa ni kuinunua nyimbo hiyo ili niiweke katika albam mpya ya bendi yangu lakini hapa kati palitokea misunderstanding baina ya Misambano na baadhi ya wasanii wa bendi yangu ndio maana unaona malumbano hayo yote yanaendelea ndugu yangu.
UBUYU WA TAARAB:- Kuna taarifa kwamba Misambano alipanga akuuzie nyimbo yake kwa kiasi cha shilingi milioni mbili na ukawa umeshampatia laki nne kama sehemu ya malipo ya wimbo huo lakini mpaka sasa wewe ndio umekiuka makubaliano na yeye hayupo tayari kuzirudisha pesa hizo, Una lolote la kusema juu ya hilo?.
MKURUGENZI G5 MODERN TAARA HAMISI SLIM. |
"HITIMISHO".
Mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Tunapenda kutoa ushauri kwa pande zote mbili kwamba ni vyema wakae chini kuzungumzia tofauti zao hizi ili kuswafiana nia sababu sanaa ni sawa na bahari kubwa, katika bahari kuna kila kiumbe na wanategemeana kwa mambo flani flani, hivyo basi Misambano na Slim ni lazima muondoe tofauti zenu ili kuweka mambo sawa....Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni