TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 30 Januari 2015

KHADIJA OMARY KOPA NA BENDI NZIMA, KUVAMIA MIKOA YA MTWARA NA LINDI VALENTINE'S DAY!!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                      Kampuni ya Spider Entertainment ya jijini Dar-es-salaam, chini ya mkurugenzi wake Mwantumu Ngoda imeamua kupeleka burudani ya Taarab toka bendi ya Ogopa Kopa Classic chini yake malkia wa taarab nchini Tanzania Khadija Omary Kopa katika mikoa ya kusini yaani mtwara na lindi katika sikukuu ya wapendanao yaani "Valentine's Day".

HII NDIO POSTER'S YA NEWALA.
         Ratiba inaonyesha kwamba Ogopa Kopa Classic Bendi itakuwa na show tatu takatifu kabisa, siku ya tarehe 13/02/2015 Ndani ya mkesha wa Valentine's Day wataanzia wilayani Newala ndani ya ukumbi wa Umoja Social Hall uliopo Newala mjini, Siku ya tarehe 14/02/2015 Siku yenyewe haswa ya wapendanao Ogopa Kopa Classic Bendi itashusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa kisasa uliopo mkoani mtwara uitwao Makonde Beach, ukumbi ambao upo ufukweni kabisa mwa bahari ya hindi. Siku ya tarehe 15/02/2015 Bendi hii itamaliza ziara yake katika mikoa hii ya kusini kwa kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Lindi kwa kufanya show ndani ya ukumbi wa Bwalo la Polisi, uliopo pale Lindi mjini.

HII NDIO POSTER'S YA MTWARA.
       Akizungumza na mtandao huu Malkia wa Taarab nchini tanzania Khadija Omary Kopa alisema kwamba ana miaka mingi sana hajakanyaga katika mikoa hiyo ya kusini hivyo amedhamilia kwenda kufanya mambo makubwa sana kwani anaamini ana wapenzi wengi sana katika mikoa hiyo na walimmiss kupita kiasi. nawaomba wajitokeze kwa wingi katika show hizo tatu kwani ninakuja na Bendi yangu nzima kwa mara ya kwanza haijawahi kutokea!, hii si yakukosa watapata bahati ya kuwaona Young Hassan Ally, Hanifa Maulidi "Jike la Chui", Zena Mohamedy, Black Kopa, Shadya Shombembe na wengineo wengi. Nyimbo zote za zamani walizozizowea zitapigwa na pia nyimbo zetu mpya pia tutazitambulisha rasmi na tutaziimba "LIVE".

         Wapenzi na wadau wa Malkia huyo wanaombwa kufika kwa wingi sababu khadija kopa ni mtu adimu hivyo wajitokeze kujumuika nae kwa pamoja na kufurahi nae ndani ya sikukuu ya Wapendanao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni