Mpiga kinanda maarufu ambae anafanya shughuli zake za muziki nchini Oman Amour Salehe Zungu, tayari ameingia nchini Tanzania na tetesi zilizozagaa jijini ni kwamba msanii huyo amejiunga na bendi ya Ogopa kopa ambayo inamilikiwa na malkia wa taarab nchini tanzania Bibie Khadija Omary Kopa.
Kama ilivyo desturi ya mtandao huu, pindi habari kama hizi zinavyotufikia basi ni lazima tumsake muhusika ili authibitishie Umma wa watanzania hususani wapenzi wa taarab kwamba je ni kweli UBUYU huu?. Mahojiano yetu yalikuwa hivi:-
AMOUR SALEHE ZUNGU-KIKAZI ZAIDI. |
AMOUR SALEHE ZUNGU:- Hapana hizo tetesi sio za kweli ndugu yangu, kilichopo ni kwamba mimi baada ya kurejea nchini nilimfahamisha Mama yangu Khadija Kopa kwamba nipo nchini kwa mapumziko ya muda mchache, Yeye akaniambia anataka tutengeneze wimbo mmoja ambao ataimba yeye mwenyewe na mimi kupiga kinanda, lakini kwamba nimejiunga moja kwa moja hapana kaka.
UBUYU WA TAARAB:- Unaweza kutudokeza jina la wimbo ambao mnatarajia kuutengeneza wewe pamoja na malkia?.
AMOUR SALEHE ZUNGU:- Mpaka sasa kiukweli sijui huo wimbo utaitwaje, ila kikubwa tuwe na subira muda utakapofika kila kitu kitakuwa wazi tu.
Huyo ndio Amour Salehe Zungu amefunguka kutokana na yale mengi yanayozungumzwa juu yake, ni matumaini yangu wasomaji wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com mtakuwa mmefaidika kwa majibu hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni