Kalieni viti sio umbea ni Songi linalofanya vizuri sana kwa sasa kupitia vituo mbalimbali vya redio na televisheni kwa Tanzania na hata nchi za jirani yaani Kenya, Uganda, Comoro, Burundi na hata Rwanda, Wimbo huu ambao upo katika bendi ya Wakaliwao Modern Taradance chini yake mkombozi Thabit Abdul, umeimbwa nae mwanadada Hamuyawezi Kondo.
HAMUYAWEZI KONDO- MUIMBJI WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE. |
UBUYU WA TAARAB:- Hamuyawezi mambo vipi?.
HAMUYAWEZI:- Poa inakuwaje kaka wa mie?
UBUYU WA TAARAB:- Poa!..sasa Hamuyawezi, kuna taarifa zimetufikia hapa ofisini kwetu kwamba wewe na Asya Mariam hamuelewani kabisa hadi inafikia hamsalimiani, tatizo kubwa ni nini haswa?.
HAMUYAWEZI:- Haha haha haaaaa!!, ni kweli kaka hizo taarifa lakini mimi tatizo haswa silijui labda nikusimulie japo kidogo tu, Mimi na Asya ni waimbaji wa Wakaliwao lakini mimi nimeanza kabla yake ndipo yeye akafuata, nimekuwa nikimsikia katika mahojiano yake mbalimbali anayoyafanya kupitia vyombo vya habari akinituhumu mimi na Boy friend wangu kwamba tumekuwa tukimwambia yeye kwamba hajui kuimba, sikweli, tatizo lipo katika kazi zetu tu! amekuwa akisema kuwa mimi napendelewa na Thabit Abdul tena kwasababu ya wimbo wa kalieni viti sio umbea hapo ndipo kwenye kiini cha tatizo!.
UBUYU WA TAARAB:- Je kwa sasa mnapokutana katika show zenu huwa mnasalimiana au kila mmoja na hamsini zake?.
ASYA MARIAM- MUIMBAJI WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE. |
UBUYU WA TAARAB:- Uongozi wa bendi yako wanalijua hili? na kama wanalijua wamelishughulikia kwa kiasi gani?.
HAMUYAWEZI:- Uongozi unajua na walijaribu kulisawazisha lakini naona hali inaendelea kuwa tete! nawashauri waache tu ili mradi kazi yao inafanyika basi hakuna shida!.
UBUYU WA TAARAB:- Je upo tayari kupatanishwa wewe na Asya ili muwe kama zamani? sababu hasama hazifai ukizingatia mnafanya kazi bendi moja!.
HAMUYAWEZI:- Sikuzote waswahili wanasema moyo ni kichaka cha siri, hilo siwezi kulizungumzia kaka.
UBUYU WA TAARAB:- Ahsante sana Hamuyawezi kwa ushirikiano wako, tutakapokuhitaji tena usisite kutupatia ushirikiano wako Dada.
THABIT ABDUL- MKURUGENZI WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE. |
Ubuyu wa taarab ulivuta waya mpaka kwa Asya Mariam ili nae azungumzie kwa upande wake imekuwaje? lakini simu yake haikuwa inapatikana mpaka tunaingia mitamboni, ila kama ilvyokawaida ya mtandao huu tunawaahidi wasomaji wetu kwamba tutamtafuta Asya Mariam ili nae azungumze kwa upande wake. Ila ushauri wa bure kwa viongozi wa Wakaliwao wasiiache hii hali iendelee kwani ni hatari kwa watu wanaofanya kazi sehemu moja alafu wakawa hawaongei ni jambo baya sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni