TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 28 Februari 2015

MUHESHIMIWA KAPTEN KOMBA MKURUGENZI WA T.O.T. BENDI AFARIKI DUNIA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

       Aliyekuwa mkurugenzi wa T.O.T Bendi na mbunge wa mbinda magharibi muheshimiwa Kapten Komba amefariki Dunia leo mida ya saa kumi jioni katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar, Chanzo kikubwa cha kifo chake inasemekana ni ugonjwa wa Pressure ingawa haijathibitishwa rasmi na madaktari waliokuwa wakimtibu ili kuokoa maisha yake.

MAREHEMU KAPTEN JOHN KOMBA.
       Akizungumza na mtandao huu makini mwanamuziki muimbaji wa bendi ya T.O.T. Abdul Misambano alithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mkurugenzi wao Marehemu Kapten Komba mida ya saa kumi jioni. aliendelea kwa kusema kuwa chanzo kikubwa cha umauti wake ni ugonjwa wa Pressure uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.
MAREHEMU KAPTEN KOMBA ENZI ZA UHAI WAKE.

MAREHEMU KAPTEN KOMBA AKIWA KATIKA VAZI LA CHAMA CHAKE CHA C.C.M.
    Taarifa rami toka kwa familia ya marehemu pamoja na uongozi mzima wa T.O.T. Bendi mtandao huu unaendelea kufuatilia na kuwajuza kila hatua itakayofikiwa mpaka mwili wa marehemu utakavyosindikizwa katika nyumba yake ya milele, mtandao huu unapenda kutoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na wasanii wote kwa ujumla Tanzania sabababu marehemu alikuwa ni msanii mkubwa ambae ameifanyia mengi makubwa na ya kukumbukwa nchi hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni