NA KAIS MUSSA KAIS.
Omary Kisila ni muongozaji wa muziki wa taarabu nchini mwenye mafanikio makubwa sana kwa sasa, mafanikio ninayoyazungumzia hapa ni ya kimuziki zaidi kulingana na utendaji wake wa kazi kwa takribani miaka mitano iliyopita mpaka sasa. Omary Kisila wa mwaka 2010 sio huyu wa 2015, kwa sasa yupo vizuri mno.
|
OMARY KISILA AKIWA KWENYE POZI. |
Nilifanya mahojiano na Director huyu, kubwa zaidi ilikuwa ni kuuzungumzia mwenendo mzima wa soko la muziki wetu huu wa taarab nchini mwetu. Je soko lipo vizuri au kuna hali ya kusuasua?. Yeye alianza kwa kusema kwamba soko halijashuka ila lipo vizuri jambo la msingi ni kwa serikali kutia nguvu zake ili kuweza kuboresha zaidi soko la muziki huu naamini kupitia wizara husika. kila jambo litakwenda sawa, lakini kwa sisi wenyewe watu wa taarab kamwe hatuwezi kufanya lolote niamini niyasemayo.
Kitu kingine sisi wasanii hatujitambui na wala hatujui thamani yetu kwa jamii, msanii anaenda kupiga open show! kiingilio kinywaji alafu siku inayofuata anaweka show kwenye ukumbi fulani kiingilio na pesa, hakuna atakae kuja!...afuate nini wakati akikutaka atakupata kwa soda ya elfu moja tu!, wakati nipo Zanzibar Stars tulikuwa na msimamo haukuwepo upuuzii kama huu wa sasa!. Open show zinauwa thamani ya bendi za Taarab na sisi wasanii kwa ujumla wake.
|
OMARY KISILA HAPA AKIWAJIBIKA KWENYE KINANDA. |
Na vipi kuhusu maadili katika tungo nyingi za taarabu hapa nchini, zinazingatia uadilifu katika jamii au watunzi wanalipua zaidi?.Alijibu, Kwanza wadau na wapenzi wanapaswa kujua kwamba kwa sasa kuna aina mbili za utunzi katika muziki wetu wa taarab nchini, kuna"tungo tata" na "mashairi ya milingamo"mashairi haya ya milingamo ni kama vile nyimbo za Fimbo ya mungu,Lauchungu Halisahauliki na Mti wa ridhiki ulioimbwa na Marehemu Mariam Hamisi. Mashairi yenye tungo tata ndio haya yanayoimbwa na kupendwa kwa sasa! nyimbo za kutiana vidole machoni, hii sio taarab! Hapa kuna ulazima mkubwa kwa serikali kutia nguvu zake na kurudisha ile sheria ya kuanza kuhakiki nyimbo au mashairi kabla hazijaenda hewani au kurekodiwa.
|
ANAITWA OMARY KISILA- DIRECTOR. |
Kwa kumalizia Je kwa sasa wewe ni msanii wa bendi gani maana umekuwa ukionekana katika bendi nyingi ukizitumikia! hebu waeleze mashabiki wako upo bendi gani?. Mimi sina bendi na nipo huru kwenda bendi yoyote ile kufanya kazi, nakaribisha bendi zi
je na tutafanya kazi kwa makubaliano rasmi.
Hayo yalikuwa mahojiano kati ya mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com mtandao bora wa taarab kwa sasa hapa nchini sambamba na Director maarufu wa muziki huu nchini Omary Kisila.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni