Aliekuwa msanii wa bendi ya Dar modern taarab Abuu mgeni, amemshushia tuhuma nzito Adam Mlamali kwamba yeye ndio chanzo na sababu ya bendi hiyo kutokufanya vizuri kwani amekuwa akiweka matabaka katika bendi hiyo kwa kuwakumbatia baadhi ya wasanii haswa wale aliopendekeza yeye waletwe pale na kuwadharau wale aliowakuta katika bendi hiyo.
Pia ametanabahisha kwamba hata ile hali iliyotokea kipindi cha nyuma kwa wasanii 13 kufukuzwa akiwemo na yeye mwenyewe katika bendi hiyo ni moja ya fitina za Mlamali kutaka wasanii aliokuja nao yeye wanabaki na wa zamani wote kuondolewa kwa makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu tena yakupandikiza kwa makusudi!.
Mtandao huu ulipopata tuhuma hizi nzito ulimtafuta Mlamali na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:-
ABUU MGENI, ALIEKUWA MPIGA KINANDA WA BENDI YA DAR MODERN TAARAB. |
UBUYU WA TAARAB:- Muheshimiwa Mlamali kwanza kabisa shikamoo!, nimekufuata kuna tuhuma zimeelekezwa kwako na msanii mmoja aitwae Abuu Mgeni, yeye anasema kwamba wewe ndio chanzo cha bendi ya Dar modern kutofanya vyema mpaka sasa, sababu umekuwa na ubaguzi ndani ya bendi hiyo kwa kuwapendelea wasanii ambao umewaleta wewe je ni kweli?.
MLAMALI:- Marahaba!, kwanza kabisa nazikana hizo tuhuma sio kweli, mimi ni mtu na heshima zangu, nimeletwa hapa Dar modern kwa minajili ya kufanya kazi na wala mimi sihusiki na kufukuza wala kusimamisha wasanii katika bendi hii.
UBUYU WA TAARAB:- Abuu Mgeni anasema hata pale lilipotokea tatizo la wao kufukuzwa bendi, wewe na wasanii wako ndio sababu kubwa!, wale wasanii uliowaleta wewe walikuwa wakimtumia sms bosi kumueleza kinachoendelea huko safarini sababu yeye hakuwa amesafiri mlipokuwa mnapiga je ni kweli?.
DAR MODERN WAKIFANYA YAO STEJI. |
MLAMALI:- Hakuna kitu kama hicho! kufukuzwa kwa wasanii wale kulitokana na utovu wa nidhamu, na kwenye bendi kuna viongozi ambao tulikuwa nao safarini, mfano meneja wao na viongozi wengine waandamizi. Sasa yeye anaposema wasanii walituma sms kwa bosi sio kweli, kwani viongozi wao hawakuwa wanaona kinachofanyika?.
UBUYU WA TAARAB:- Mwisho una lipi la kusema kwa wasanii wako wa Dar modern, viongozi wenzio na hata Abuu Mgeni!.
MLAMALI:- Mimi labda nimueleze Abuu mgeni kwamba, nipo katika taarab miaka mingi sana, huwa sina tatizo na mtu kwahiyo asipende kunichafua kwa tuhuma zisizo na kichwa wala miguu. Ushauri kwa wasanii wa Dar modern nawaomba tuwe na mshikamano na wala wasiyumbishwe na maneno ya "agongae mlango huku kufuli limachoni mwake",
WAIMBAJI WA DAR MODERN WAKIWAJIBIKA STEJINI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni