TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 13 Aprili 2015

BAADA YA MAHABA NIUE...SASA JIANDAE KUPATA KANING'ANG'ANIA NG'ANG'ANI TOKA KWA MZEE YUSUPH.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Ukizungumzia wasanii wa muziki wa taarab wanaofanya vizuri kwa sasa hapa nchini tanzania basi ni lazima jina la Mzee Yusuph mkurugenzi wa Jahazi modern taarab litakuwa ni miongoni mwa hao!.Baada ya kutoa wimbo wa Chozi la mama na Mahaba niue, sasa jiandae kusikia kibao kipya kabisa toka kwa Mzee Yusuph kiitwacho "Kaning'ang'ania ng'ang'ani".


MFALME MZEE YUSUPH AKIWA NA MKEWE LEYLA NA DADA YAKE KHADIJA YUSUPH.

     Huu ni wimbo wa mapenzi tena wenye maneno matamu kabisa ya kumtoa nyoka pangoni, Mfalme hapa anawaambia wale wenye roho za husuda na penzi lake kwamba wanajisumbua tu kwani sweet kamkubali, kamganda tena kamng'ang'ania ng'ang'ani, ni mashairi yaliyo na mafunzo kwa jamii.


 Director wa bendi ya Jahazi modern taarab Mohamedy Mauji akizungumza na mtandao huu bora wa taarab nchini tanzania alisema kwa sasa wanaanda nyimbo zaidi ya tatu mpya kali na safari hii kuna uwezekano mkubwa tukamtoa muimbaji mmoja chipukizi aitwae "Mishi" ili wapenzi na wadau wajue uwezo wake katika uimbaji.

 Kama ilivyo ada ya mtandao huu, tunamtakia mfalme mzee yusuph maandalizi mema ya utengenezaji wa albam ijayo ambayo wadau wanaamini itakuwa ni nzuri sana sababu mfalme amekuwa habahatishi katika tungo na nyimbo zake kwa ujumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni