Bendi inayokuja kwa kasi ya ajabu kwa sasa katika tasnia ya taarab nchini, Ogopa Kopa Classic chini yake malkia wa taarab bibie Khadija Omary Kopa siku ya leo ijumaa wanatarajia kushusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa Shangilila Perugina uliopo mkoano Dodoma.
MALKIA WA MIPASHO NCHINI KHADIJA OMARY KOPA. |
Akizungumza na mtandao huu muimbaji wa bendi hiyo ambae pia ni mtoto wa malkia wa mipasho nchini anaefahamika kwa jina la kisanii Black Kopa alisema bendi imeondoka leo asubuhi hapo Dar na tutakuwa na show tatu, ya kwanza ndio hiyo ya Dodoma mjini ambayo itakuwa leo ijumaa, ya pili na ya tatu zitafanyika singida na kondoa, baada ya hapo jumatatu ijayo bendi itarejea Dar ili kuendelea na maonyesho yetu ya kila wiki kama kawaida.
WAIMBAJI WA OGOPA KOPA WAKIWA STEJI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni