TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 18 Aprili 2015

GUSAGUSA MIN BEND NDANI YA HUGO HOUSE KINONDONI JUMAPILI HII NA KILA JUMAPILI.



NA KAIS MUSSA KAIS
 

WAPENZI wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini Jumapili hii ya Aprili 19/4/2015,  wanatarajiwa kupata burudani safi na ya aina yake  kutoka kwa kundi la Gusagusa min bend,  ndani ya ukumbi wa Hugo house uliopo  kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa onyesho hilo, kwa kushirikiana na Hugo house,  amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi kuufurahia, kukumbushiana enzi za muziki wa mwambao wa taarab wa zamani.

Asia Idarous alisema onyesho hilo pia litakuwa ni la kila siku ya Jumapili katika ukumbi huo wa Hugo house, eneo lenye mazingira safi huku kiingilio kikiwa cha kawaida cha sh 5,000 tu!.Tumeamuakuhamisha onyesho hilo tokea safari canival kawe mpaka hapa Hugo house kinondoni kutokana maombi ya wateja walio wengi.

ASYA IDAROUS KHAMSIN MKURUGENZI WA FABAK FASHION'S.

“Kila Jumapili Gusagusa min bend watakuwa wakitoa burudani ya nyimbo za mwambao hasa zile zilizokuwa zikipendwa,  kuanzia saa saa tatu usiku hadi majogoo,” alisema Asia Idarous.

Asia Idarous pia alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zimekuwa gumzo kipindi hicho ni pamoja na Nidhibiti, Nisubili hadi lini, Pete, kama ni rahisi, Kanakupa, ‘Pendo kitu cha hiari’, Dunia ina fisadi, Kibali, Kasha na nyingine nyingi. Aidha aliongeza kuwa Hugo house itakuwa ni kiota cha burudani ya miziki hiyo ya zamani huku usiku huo ukiwa unajulikana kama ‘OLD IS GOLD’ na watu mbalimbali wakitarajiwa kukutana hapo na kubadilishana ya zamani alimalizia kusema mkurugenzi huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni