TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 18 Aprili 2015

PRINCE MWINYIJUMA MUUMIN KUTOA LA MOYONI KESHO SAA NNE ASUBUHI NDANI YA E FM REDIO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

MWINYIJUMA MUUMIN AKIWA NA MTANGAZAJI WA E FM ISSA NANDUMBI.
               Ule wakati uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa wa Mwinyijuma muumin kocha wa dunia kuweka bayana yale yanayo msibu katika mtima wake kwa siku nyingi umewadia, ni siku ya kesho jumapili ndani ya E FM REDIO katika kipindi cha taarab kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa saba mchana.

      Akizungumza kwa kujiamini sana Muumin alisema siku ya kesho ndio jamii itajuwa nini na naanisha katika hili la kuweka wazi nilichonacho moyoni, ni muda mrefu sana nimekuwa nikisumbuka juu ya hili jambo, ila yoyote kwa yote nawaomba wadau wangu tuwe sote ndani ya E FM kesho mapema saa nne asubuhi nitafunguka kila kitu.

   Muumin anataka kuzungumza nini, mbona ameonekana ni msiri sana juu ya jambo hilo? mimi na wewe hatujui, kikubwa tuendelee kusubiria kesho tumsikie mwenyewe akizungumzia jambo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni