TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 19 Aprili 2015

UBINAFSI WA VIONGOZI WA TAARAB, NDIO CHANZO CHA KUSHINDWA KUKIFUFUA CHAMA CHAO NCHINI.






NA KAIS MUSSA KAIS.

                     Asalaam aleykum wapenzi wasomaji wangu, habari za week-end!, leo hii tumekutana tena katika ile sagment yetu ya makala ya wiki ambayo huwa naileta kwenu kila Jumapili panapo majaaliwa yake mola, leo napenda nizungumzie "Chama cha muziki wa taarab nchini na majaaliwa yake kiujumla".


     Muziki wa taarab nchini umekuwa ukiendeshwa kienyeji enyeji zaidi jambo linalopelekea hata wasanii husika wa fani hii kudharaulika na serikali yenyewe hata jamii inayoizunguka. Mara ngapi muheshimiwa Rais amekuwa akifanya sherehe nyumbani kwake lakini vikundi vinavyopata mialiko ni bongo freva na bongo movies, taarab wanaachwa nyuma sana! mimi siwezi kumlaumu muheshimiwa Rais juu ya hili! tatizo kubwa lipo kwa viongozi wenyewe wamejaa unafiki, umimi, chuki zisizo na msingi, usengenyaji na roho mbaya miongoni mwao jambo linalochangia kurudisha nyuma mchakato wa kukifufua chama cha taarab nchini.


       Katika mchakato wa kwanza juu ya kukifufua chama hiki, mimi mwenyewe nilikuwa ndio katibu wa vikao ambavyo vilidumu takribani vikao vinne tu, baada ya hapo washiriki walianza kupungua mmoja mmoja bila kutoa sababu za msingi za kufanya hivyo mpaka tukabakia wachache na mbio za kukifufua chama hicho  kuishia njiani.Miezi mitatu iliyopita mchakato ulifufuliwa tena na wadau wakubwa katika muziki huu ambao ni Mkurugenzi wa T motto Amin Salmin, mkurugenzi wa bendi ya Segere Siza Mazongela na mkurugenzi wa Kongamoyo bendi anaetambulika kwa jina la Iqbal, hawa walikuwa ni waanzilishi tu wa mchakato huu then baadae wahusika wote wangeitwa kwenye kikao rasmi  kupitia Baraza la sanaa taifa [BASATA] ili ikiwezekana wachaguliwe viongozi wa muda lakini mpaka sasa hakuna kinachojulikana!, swali la msingi linakuja ni jambo gani haswa linalofanya mchakato huu kutofikia malengo kila unapoanzishwa?.


         Viongozi wa bendi za taarab kumbukeni kuwa siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, hebu acheni ubinafsi na kujitunisha vifua mbele kwa mafanikio ya hapa machoni! Kaeni pamoja ili kukifufua chama cha muziki wetu huu nchini kwani faida zake ni nyingi kuliko hasara kama mnavyodhania, mialiko mingi imekuwa ikifika "Basata" ili bendi ziweze kwenda nje kufanya matamasha lakini nini kinafanyika zaidi ya kuteua vikundi vya ngoma za asili na kuwakilisha nchi huko ughaibuni?.


       Wasanii wa taarab wamekuwa wakipoteza maisha kwa magonjwa mbalimbali karibia kila mwaka lakini kama chama kingekuwa hai kungejengwa msingi imara wa kuweza kuwakumbuka wenzetu waliotangulia mbele ya haki japo kwa dua ya pamoja kila mwaka mara moja. Mashindano ya "KILI MUSIC AWARD'S" yanayoendelea nchini chama kingeweza kuwa na sauti ya kupanga kategoli muhimu tunazozitaka ili kuweza kuwainua waimbaji wachanga na kupata hamasa zaidi ya kuendelea kufanya muziki huu pindi wapatapo  tuzo hizo.


       Ushauri toka katika meza ya habari ya blog hii bora nchini tanzania ni kwamba, viongozi kwa pamoja rudini katika meza ya majadiliano ili kukinusuru kizazi kijacho ambacho kinaonekana wazi kukosa dira na muelekeo wa kuunyanyua na kuukuza vyema muziki huu wenye historia kubwa nchini mwetu, wakati ni huu wala hamjachelewa aanzeni sasa na wadau naamini watatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha hili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni