TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 20 Aprili 2015

PRINCE MUUMIN:- WENYE PESA WALINIPORA MKE WANGU SADA SALEHE NA KUNIFANYA NIYUMBE KIMUZIKI!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                Siku ya jana jumapili katika kipindi cha "ladha tamu" ndani ya E fm redio Prince mwinyijuma muumin au kocha wa dunia aliweka wazi yaliyopo moyoni mwake na kufanya umma wa wasikilizaji wa redio hiyo kuumizwa sana na maneno ya uchungu aliyokuwa akiyasema Muumin.


MWINYIJUMA MUUMIN

       Akizungumza kwa hisia kali jambo lililotafsiriwa kwamba alikuwa akivuta picha ya matukio ya nyuma  yaliyomkuta katika ndoa yake hiyo Muumin alisema, ana kumbuka wazi kabisa jinsi ndoa yake na Sada Salehe ilivyokuwa gumzo kipindi kile, ndoa ile ilinigharimu pesa nyingi sana haijapata kutokea!, lakini pia imenifanya kuendelea kuwa na doa kubwa katika historia ya maisha yangu, Watu wenye pesa kwa makusudi waliivunja ndoa yangu kwa kumrubuni mwenzangu na kuondoka nae.


      Sipendi sana kukumbukia hili tatizo maana limeshapita nami sasa nina mke mwingine ila imenilazimu kuweka wazi sababu wadau na wapenzi wangu walikuwa wananiuliza sana nini sababu iliyopelekea mimi kuyumba kimuziki mpaka kuwa kimya kidogo!. kwa sasa napenda nitangaze rasmi mbele ya watanzania wote kwamba nimeingia kwenye muziki wa taarab rasmi na nimeshatoa nyimbo mbili ambazo ni "Kigodoro kimelowa maji" na wimbo wangu

PRINCE MWINYIJUMA MUUMIN

mpya mwingine ambao nimeuachia hivi karibuni uitwao "Jasho la baba" nikiwa na bendi ya G5 Modern Taarab.


     Vile vile nipo chini ya meneja wangu mpya Kais mussa kais au ukipenda muite mzee wa fitina mjini, huyu jamaa anajua sana kusimamia bendi au wasanii, kupitia yeye naamini wazi hakuna atakae nisogelea kimuziki hapa ni mbele kwa mbele tu, walioanza zamani nawaambia pisha mbele Muumin anakuja, sibahatishi nakuja kiupinzani zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni