TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 21 Aprili 2015

HATIMAE GUSAGUSA MIN BENDI WAKWEA PIPA KUELEKEA UINGEREZA!!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

          Bendi yako uipendayo ya Gusagusa min bendi usiku wa jana jumanne imekwea pipa kuelekea uingereza kwa ajili ya kufanya show mbili kali na matata sana!, kama inavyofahamika wazi bendi hii huwa haina mchezo inapokuwa jukwaani.


MKURUGENZI WA GUSAGUSA MIN BENDI HASSAN FAROUK AKIWA NDANI YA NDEGE.

         Akizungumza na mtandao huu makini muandaaji wa show hizo mbili Didas Fashion mtanzania mwenye makazi yake nchini uingereza amesema maandalizi yote tayari yamekamilika na kilichokuwa kinasubiliwa ni kufika kwa Gusagusa min bendi nchini UK ili raha ziendelee.


     Nae mkurugenzi wa bendi hiyo Hassan Farouk alisema anashukuru kuweza kufanikiwa kwenda kuipeperusha vyema bendera ya Gusagusa nchini uingereza na amewaomba wadau na wapenzi wa bendi hiyo waishio nchini humo kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yao kwani wamejiandaa vyema na watapata kitu roho inapenda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni