NA KAIS MUSSA KAIS.
Wapenzi wasomaji wa blog bora ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com, leo hii tumekutana tena kama ilivyo desturi yetu kuhabarishana kupitia kipengele hiki kipya kilicho jizolea umaarufu mkubwa kwa muda mchache tu, kipengele kinachokwenda kwa jina la "Sindano tano za ubuyu wa taarab".
HII NDIO PICHA YA AMIN SALMIN NA JOKHA KASIM AMBAYO ILIZUA MANENO MENGI. |
Leo tupo nae mkurugenzi wa T motto modern taarab Amin Salmin, pamoja na mambo mengi ya bendi yake aliyoyazungumza lakini yale maswali yetu ya kizushi hayakuwa nyuma, hebu tutililike kwa pamoja katika kufahamu nini alizungumza nami, twende sawa:-
UBUYU WA TAARAB:- Mkurugenzi leo nimekufuata ofisini kwako ili kupata mawili matatu toka kwako na wadau wako waelewe!, kuna tetesi zipo mitaani kwamba ndoa yako na Jokha Kasim ni danganya toto tu wala haikuwa kweli sababu picha mlizoposti kwenye mitandao ambazo zinaonyesha Jokha Kasim kavaa shella la harusi ni siku ile ya uzinduzi wa albam ya pili ya bendi yako ambayo ilifanyika pale Dar Live mbagala Dar unasemaje?.
MKURUGENZI WA T MOTTO AMIN SALMIN. |
AMIN SALMIN:- Kwanza napenda niwadhihilishie wapenzi na wadau wangu kwamba Jokha Kasim ni mke wangu wa halali kabisa, nimefunga nae ndoa na kufuata taratibu zote za dini yetu ya kiislam, isipokuwa niliifanya ndoa ile kuwa ya siri kwasababu zangu binafsi tu!, kwa sasa naandaa sherehe kubwa ambayo itajumuisha watu wote mpaka vyombo vya habari nanyi mtakuwepo.
UBUYU WA TAARAB:- Ni kwanini umekuwa na msuguano mkubwa na Mzee yusuph, tena wewe ndio unae onekana ndio unamuanza mwenzio pamoja na bendi yako ya T motto kwa ujumla, tatizo ni kwasababu Jokha Kasim alikuwa mke wa Mzee? au mnaugomvi wa muda mrefu na mkurugenzi mwenzako?.
HILI NI GITA LA BESI LA NYUZI SITA LA AMIN SALMIN JIPYA KABISA. |
AMIN SALMIN:- Haha haha haaaa!, hapana sina tatizo na Mzee yusuph, kile unachokiona kinaendelea baina yetu ni upinzani wa kimuziki tu wala hakuna jambo tofauti na hilo, alafu watu wakae wakijua kwamba hata kama Jokha Kasim alikuwa mke wa Mzee yusuph lakini ni kipindi hicho cha nyuma! kwa sasa ni mali yangu mimi Amin salmin.
UBUYU WA TAARAB:-Bendi yako ya T motto imekuwa kimya kwa muda mrefu sasa, kila kukicha tumekuwa tukisikia tu bendi inarudi bendi inarudi! leo hii kupitia sindano tano za ubuyu wa taarab waeleze wadau wako tatizo lipo wapi? au unakwamia wapi kiongozi usaidiwe?.
HII NI MIXER MPYA KABISA NA YA KISASA ZAIDI YA AMIN SALMIN. |
AMIN SALMIN:- Wapenzi wa taarab wakae wakijua kwamba jambo lolote unapolianzisha linahitaji utulivu na umakini mkubwa, mimi nilishaanzisha bendi hii zaidi ya mara mbili na ikapotea! kwahiyo mara hii ya tatu sitaki kuona bendi yangu inapotea tena, nimejipanga vyema na waendelee kusubiri kwani muda si mrefu nitaita waandishi rasmi na kuitambulisha T motto inarejea na mikakati gani kwa mara ya tatu!.
UBUYU WA TAARAB:- Miongoni mwa wasanii wapya ambao umepanga kuwachukuwa ili kuongeza nguvu katika ujio mpya wa bendi yako yupo Khadija yusuph wa Jahazi modern taarab je ni kweli Boss?.
HII NI SETI YA VYOMBO VYA KUFANYIA "P.A." TU BARABARANI VYA AMIN SALMIN. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni