TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 23 Aprili 2015

FIVE STAR'S MODERN TAARAB WAINGIA LOCATION KUMALIZIA SHOOTING YA ALBAM YA KICHAMBO KINAKUHUSU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                  Bendi ya Five star's modern taarab chini ya mkurugenzi Ally J inatarajia kuingia Location kesho kumalizia kabisa albam yao ya "kichambo kinakuhusu" ambayo ina takribani nyimbo tano.


ALLY J MKURUGENZI WA FIVE STAR'S MODERN TAARAB.

        Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi huyo alisema anamshukuru mungu kwani wamekuwa wakiendelea vyema yeye na wasanii wake, hakuna tatizo lolote na watakapomaliza shooting ya nyimbo zao wanatarajia kueleke nyanda za juu kusini mikoa ya iringa na mbeya, watakuwa na show takribani nne, baada ya hapo watarejea Dar kabla ya kuelekea mtwara na lindi kwa maonyesho zaidi, Pia alisema kuwa Bobo mautundu ambae alifanya video ya makavu live ya Hanifa maulid ndie ambae ataifanya kazi hiyo mpya ya five stars kwa albam ya kichambo kinakuhusu.


     Alizitaja nyimbo zilizopo katika albam hiyo mpya kuwa ni:-


                1. Kichambo kinakuhusu - Mariam B.s.s.

                2. Big up my dear - Mussa kijoti.

                3. Kishtobe - Salha wa Hammer

                4.Sina ghubu - Mape kibwana

                5.Ubaya hauna soko - Mwanaida Ramadhan


Mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unapenda kuwapongeza five stars modern taarab kwa hatua kubwa waliyopiga kwani ni bendi nyingi zinatamani kufikia pale wao walipo lakini zinashindwa kutokana na menejiment mbovu ambayo wapo nayo, Big up sana mkurugenzi Ally J.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni