TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 26 Aprili 2015

NI MUHIMU KWA BENDI ZA TAARAB NCHINI KUWA NA WEBSITE ZAO BINAFSI ILI KUJITANGAZA KIMATAIFA.


NA KAIS MUSSA KAIS.

                Ndugu wasomaji wangu wa blog hii bora ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com kwanza naomba niwasalimu Asalaam aleykum kwa wale waislam wenzangu na ndugu zangu wakristo Amani ya bwana iwe nanyi!. Leo tumekutana tena katika kona hii ya makala ya wiki ili tujaribu kupeana matirio kidogo, kama ujuavyo wakati mwingine akili inatakiwa kustuliwa kidogo ili ifanye kazi kwa ufasaha.


      Kwa sasa kumekuwa na utitiri wa bendi za taarab nyingi sana hapa nchini tanzania, lakini ukijaribu kuwauliza watu waishio nje ya nchi hii ni bendi zipi za taarab anazozifahamu toka tanzania atakutajia Jahazi, Mashauzi, East african melody na zanzibar stars ambayo kwa sasa haipo kabisa katika ramani ya burudani nchini tanzania. Lakini hii yote inatokana na udhaifu wa viongozi wa hizi bendi zingine kutokujua thamani ya kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii.


    Hivi sasa Dunia imekuwa kama kijiji, habari zimekuwa zikifika kwa haraka zaidi kupitia mitandao, kuna vikundi vya ngoma za asili hapa nchini vimekuwa na utaratibu wa kuweka masuala ya kazi zao katika website na kila mwaka huwa wanasafiri ughaibuni zaidi ya mara nne au tano, lakini hapa nyumbani Tanzania wala hawana show hata moja na wala hawajulikani!. Taarab ni muziki wenye historia kubwa sana hususani katika nchi yetu ya tanzania.


    Ukisoma historia ya Tanzania muziki huu wa taarabu ulishiriki katika harakati za kudai uhuru wa nchi hii, lakini ukija katika maendeleo inashangaza kuona wanamuziki wa tasnia hii ni watu wenye maisha ya hali ya chini sana!, lakini hii yote inatokana na kutojitambua thamani yao halisi, na lawama kubwa nazipeleka kwa viongozi wa hizi bendi, nini wanafanya katika kuzitangaza bendi zao?.


     Hizo bendi ambazo nimezitolea mfano hapo juu zimefanikiwa kujulikana kwa juhudi za waandishi tu kipindi hicho, kuna baadhi zimekuwa zikijitahidi kujitutumua humu katika FB na kutengeneza magroup kiasi chake, lakini kasi ni ndogo sana, juhudi zinatakiwa ziongezeke kwa kiasi kikubwa mno katika kujitangaza!.


   Ushauri wangu kwa viongozi wa bendi za taarab, wakati umefika sasa!, wanatakiwa kuajiri mtu wa ku-deal na mitandao tu tena huyo mtu awe mzoefu anae ijua kazi yake haswa, afungue website au blog ya bendi, afungue account ya FB, afungue Group la bendi, afungue page ya bendi, afungue account ya Google, ajiunge na mtandao wa  pinterest.com na baadhi ya mitandao mingine. Baada ya hapo awe ni mtu wa kuhakikisha mitandao hiyo inakuwa na habari kila wakati zinazohusiana na Ufanisi wa bendi husika! mafanikio mtayaona yanakuja!. Hakuna uchawi katika hilo ndugu zangu. Hebu nitazameni mimi, nina muda gani tokea niichukue Gusagusa min bendi lakini angalieni maendeleo yake kupitia mitandaoni!, Wapo UK kwa sasa, na kuna show kama tatu za nje ya nchi tutazifanya mwaka huu huu apendapo mungu!. Badilikeni wakati ndio huu viongozi,waswahili wanasema kitu kizuri kula na nduguyo!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni