NA RIPOTA WAKO USWAHILINI.
Kwa sisi tuliokulia "uswahilini" Dar Es Salaam tunalitambua hili. Mdundiko. Ngoma ambayo kwa hakika ilitufanya wengi kukumbana na mengi.
Mdundiko ulikuwa ukikusanya watu wengi na tukienda mwendo mrefu na katikati ukikusanya watu ambao kwa kuwa wanaongezeka "nje" ya ulipo wewe, unajikuta uko katikati na kama ndio mtoto basi hata namna ya kujisogeza pembeni huwezi.
KUSELEBUKA NA MDUNDIKO USWAHILINI KAMA KAWA!. |
Na humo katikati unasuguliwa na majasho na vikwapa vya watu na mpaka ngoma inazimwa, unarejea nyumbani (kama hutapotea) ukiwa una harufu itayomfanya mzazi atake maelezo ya kina juu ya utokako. Maana unakuwa unanuka kama zizi. Watu mamia, vikwapa vina "harufu mbalimbali" tofauti ya kuachia "pwiaaa" na wengine kuoga ni mbinde kwao. Yaani ni mshikemshike tu
Kibaya zaidi ni kuwa "tulishakatazwa" kuufuata maana watoto wanapotea saana lakini mara zote tukiuona tunajiaminisha kuwa tutaucheza kwa dakika chache alafu tutarudi. Ukija shituka, unafika nyumbani wakati wanakulachakula cha usiku!.
Na sheria ya nyumbani ni kuwa kama giza limelazimisha taa ziwashwe, ina maana hustahili kuwa nje [lazima ulambwe bakora] Na kwa wengine hii ikasababisha mengine mengi. Wapo wanaopata wanaowataka (wapenzi wapya) na wapo wanaoachwa kwa kufuata yasiyotakwa.
NGOMA YA MDUNDIKO IKIKATIZA MITAANI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni