NA KAIS MUSSA KAIS.
+255657036328.
Ni jumatano ingine tena tumekutana wajanja katika sindano tano za ubuyu wa taarabu kama ilivyo kawaida yetu, leo tupo na Mwinyi mkuu wa le grand utalii bendi, ambae kuna habari zimezagaa jijini kwamba amemuoa muimbaji mwenzie katika bendi hiyo aitwae Maina Thadei je kuna ukweli wowote katika hili? ungana nami katika sindano tano za ubuyu wa taarabu utajua kila kitu.
UBUYU WA TAARAB:- Mwinyi mkuu mambo vipi!, hongera sana kwa kazi nzuri za utalii bendi, kuna ubuyu umezagaa jijini kuwa umemuoa Maina Thadei, lakini watu wamekuwa na wasiwasi kwamba si kweli hamjafunga ndoa ila ni project ambayo mnatarajia kuifanya siku za usoni je lipi la ukweli hapa?.
MWINYI MKUU NA MKEWE MAINA THADEI WAKIWA NA FURAHA SIKU YA NDOA YAO!. |
MWINYI MKUU:-Kwanza nikushukuru kwa pongezi zako kaka, pili naomba watu waelewe kuwa Maina Thadei nimemuoa kweli na kwa sasa ni mke wangu wa halali kabisa, nimemuoa tarehe 7/5/2015, tuliamua kuifanya ndoa yetu iwe ya kawaida ili kukwepa macho ya husuda unajua katika hii dunia huwezi kupendwa na kila mtu.
UBUYU WA TAARAB:- Kuna tetesi zimetufikia kuwa wakati upo na mahusiano na Maina Thadei, pia ulikuwa unatoka na muimbaji mmoja wa wakaliwao modern taradance [jina kapuni kiusalama zaidi] ambae alikuwa akifika mara kwa mara hapo mazoezini kwenu MRC mikocheni ni kweli?.
MWINYI MKUU:- Haha haha haaaa! hapana bwana sio kweli, hata mimi hizo tetesi pia nimezisikia lakini ni uzushi tu wa walimwengu, hawa madada wa wakaliwao tunaheshimiana sana kamwe haliwezi tokea hilo jambo, nampenda sana mke wangu Maina!.
MREMBO MAINA THADEI, MKE HALALI WA MWINYI MKUU. |
UBUYU WA TAARAB:- Umekuwa ukifuatwa fuatwa sana na wanawake wakikutaka kimapenzi haswa katika kumbi mbalimbali mnazopiga, unadhani utaweza kuilinda ndoa yako kwa kutomsaliti mkeo kutokana na vishawishi vinavyokukuta?.
MWINYI MKUU:- Ni kweli nimekuwa nikifuatwa na mashabiki, kwanza nashukuru alafu ata yule anaesema ananipenda simchukii kwani amefikisha hisia zake kwangu lakini ukweli utabaki pale pale hao ni mashabiki zangu tu, na Maina Thadei ni mke wangu kamwe sitomsaliti I swear!.
UBUYU WA TAARAB:- Maina Thadei ni msichana mzuri sana naamini wapo wanaume wenye pesa zao watavutiwa nae na watapenda kuwa nae kimapenzi, je umejipanga vipi katika kukabiliana na khali hiyo ukizingatia mnafanya kazi bendi moja kwa sasa?.
MWINYI MKUU AKIWAJIBIKA STEJINI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni