Mwanamuziki Hammer Q ambae alitamba sana na wimbo wake pembe la ng'ombe wakati akiwa katika bendi ya Dar-es-salaam modern taarab ya jijini Dar, kwa sasa yupo nchini Uganda katika jiji la jinja akiendeleza harakati zake za kimuziki haswa wa taarab ili kuhakikisha muziki huu unakuwa na wapenzi wengi na unafahamika zaidi hapa afrika mashariki.
HAMMER Q!. |
Mtandao huu ulinusanusa na kufanikiwa kulivumbua hili na kama mjuavyo wasomaji wangu ubuyuwataarabutz.blogspot.com ni mtandao makini ambao umekuwa ukiwaletea habari adimu kabisa ili muweze kuelewa kinacho endelea kwa bendi hata na wasanii tofauti tofauti, mazungumzo yetu na Hammer Q yalikuwa kama ifuatavyo!:-
UBUYU WA TAARAB:- Hammer Q habari yako kaka, naona umeadimika sana ndugu yangu, kuna taarifa tupo nazo hapa ofisini kwamba kwa sasa upo nchini uganda ni kweli? na kama ni kweli ni jambo gani haswa limekupeleka huko? mashabiki zako na watanzania kiujumla wangependa kujua.
HAMMER Q:- Ni kweli ndugu yangu nipo nchini uganda kwa sasa katika mji wa jinja na nimepata mualiko toka kwa marafiki zangu ambao wameamua kuanzisha bendi za muziki wa taarab hapa nchini uganda na wao pia ni waganda, kwahiyo walikuwa wanataka kupata uzoefu zaidi ni jinsi gani sisi tanzania tunauendesha muziki huu mpaka kufikia mafanikio kwa afrika mashariki.
HAMMER Q AKIWA NA WENYEJI WAKE NCHINI UGANDA. |
UBUYU WA TAARAB:-Unaweza kuwaeleza wasomaji wa mtandao huu ilikuwaje mpaka iwe Hammer Q na wala sio mwingine yeyote katika tasnia hii ya taarab nchini tanzania?
HAMMER Q:-Hawa rafiki zangu walinitafuta kupitia facebook kama miaka miwili hivi iliyopita, wakanieleza kuwa wanataka kufanya muziki wa taarab ila kuna baadhi ya mambo hawayajui mfano kama lugha yetu ya kiswahili na njia za uimbaji wa taarab, walinialika mara ya kwanza kwa ajili ya kuja kuona wanachokifanya, nikaja nikaona wanachokifanya nikagundua kipo tofauti sana na sisi huko tanzania.
HAMMER Q ON THE STEJI NCHINI UGANDA. |
UBUYU WA TAARAB:- Ni tofauti zipi haswa ambazo wewe uliziona, na mpaka sasa kuna bendi za taarab nchini uganda ambazo zimeanzishwa zinafanya muziki huu?
HAMMER Q:- Yah! mpaka sasa uganda kuna bendi mbili tu za taarab, nazo ni Blue star's modern taarab ambayo inaongozwa na Mbatacky Ally, Abdallah Shizo, Faizo, Ziri, Fatmei na ina msichana mmoja tu, vile vile kuna bendi ingine inaitwa Alwatan modern taarab ambayo inaongozwa na Akbar Fadhaal, Nabil Said, Gadafi Said, na Omary, Tofauti iliyopo ni kwamba waimbaji wao wengi ni wanaume, wasichana imekuwa adimu tofauti na sisi tanzania.
UBUYU WA TAARAB:- Nikupongeze kwa harakati zako kaka, ulipogundua mapungufu hayo ni hatua zipi ulizichukua katika kuwasaidia wewe kama mzoefu wa muziki huu?.
BANGO LA BENDI YA BLUE STAR'S MODERN TAARAB UGANDA. |
HAMMER Q:- Hata kama mimi siwezi kupiga chombo chochote katika muziki wetu huu lakini najua njia za muziki huu kuanzia upigaji mpaka uimbaji, hivyo nilianza kwa kuwapa melody za uimbaji wa taarab mpaka upigaji na nashukuru wanaelewa vyema kabisa sababu asilimia kubwa muziki wamesomea tofauti na sisi huko tanzania.
UBUYU WA TAARAB:- Unawezaje kuzisaidia bendi zote mbili kwa wakati mmoja, hakuna malalamiko au majungu flani kama tulivyozoea kwa bendi zetu hapa tanzania?.
WAPIGA KINANDA WA BLUE STAR'S MODERN TAARAB UGANDA WAKIWA KAZINI |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni