TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 14 Juni 2015

KILI MUSIC AWARD'S IMESHAPITA, WADAU TUBADILIKE KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.


NA KAIS MUSSA KAIS.

         Kile kinyang'anyiro cha kupata wasanii bora na bendi bora za taarab nchini tanzania kinachojulikana kama kilimanjaro music award's kimefikia tamati jana usiku na kupata washindi wake ambao walitangazwa na kupewa tuzo mbele ya haraiki ya watu. napenda kuchukuwa nafasi hii kuzipongeza bendi za Jahazi modern taarab na Mashauzi modern taradance kwa kuweza kushinda siku ya jana kwa vipengele tofauti.


     Jambo kubwa lililonisukuma kuandika makala hii ni kuwaasa wadau na wapenzi wa taarab kuacha lugha za matusi na kejeli aidha kwa wasanii au wao kwa wao!,hili jambo linafanya jamii kutuona sisi wadau na mashabiki wa muziki huu wa taarab ni watu wenye tabia za ajabu ambazo hazifai kufumbiwa macho kabisa!. hebu tupendane tupeane ushauri kwenye tatizo hata mmoja wetu anapofikwa na jambo basi tuweze kulitatua kwa pamoja!.


      Mimi binafsi yangu sioni umuhimu wa kuendelea kutukanana mitandaoni kwa sababu ya mapenzi ya bendi fulani au msanii fulani, ushabiki upo tokea zamani lakini huu wa kuchafuana mitandaoni umevuka mipaka haipendezi kiukweli, msidhani mnavyokuwa mnatukanana watu wazima na viongozi hawaoni kinachoendelea! la hasha! wanaona, kinachotokea na kutudharau na kutuona hatuna thamani yoyote mbele ya jamii. napenda nitolee mfano wa lile bifu la mzee yusuph na thabit abdul pale mzee yusuph aliposikika ktk  redio flani akimuonya thabit abdul kuacha kupiga nyimbo zake pindi anapokuwa katika jukwaa la wakaliwao modern taradance!


   Wadau walirumbana sana humu mitandaoni kati ya team jahazi na team wakaliwao mpaka kufikia kutukanana matusi ya nguoni, lakini siku ya onyesho la Mashauzi classic na Jahazi modern taarab pale tlavetine niliwashuhudia kwa macho yangu thabit abdul na mzee yusuph wakizungumza kwa pamoja huku wakigongeana kwa furaha kubwa utadhani hakuna lolote linalo endelea!...mfano huu unakupa picha gani wewe kama mdau mwenzangu?, hebu badilika malumbano hayana faida kwako!.


    Katika kuuelekea mwezi huu mtukufu wa Ramadhan nawaomba wadau na wapenzi wote wa taarab afrika mashariki na kati kuacha malumbano na matusi ambayo asili yake ni kubomoa na wala si kujenga, kila mmoja kwa imani yake amrudie mungu wake na kutubu madhambi ambayo aliyatenda, najua hakuna binadamu alie mkamilifu, basi tuchukue nafasi hii kuacha kabisa yale yote yasiyo mpendeza mungu....AHSANTENI SANA!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni