Bendi yako ya Ogopa kopa classic chini ya malkia wa mipasho nchini Tanzania Khadija Omary Kopa sambamba nae Msagasumu wanatarajia kushusha burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wa kwetu pazuri mbagala jijini Dar ili kuwapa raha wakazi wa mbagala na vitongoji vyake.
OGOPA KOPA CLASSIC BENDI. |
Akizungumza na mtandao huu malkia huyo wa mipasho nchini alisema siku hiyo nawaomba wapenzi na mashabiki wetu wa mbagala wajitokeze kwa wingi kwani bendi yangu itapiga nyimbo zote mpya zinazotamba kwa sasa katika vituo mbalimbali vya redio nchini, bila kusahau tutapiga zile nyimbo za zamani zangu mwenyewe kama vile full stop, mjini chuo kikuu, ngwinji na nyinginezo nyingi sana.
KHADIJA OMARY KOPA MALKIA WA MIPASHO NCHINI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni