TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 8 Juni 2015

G5 MODERN TAARAB, YAMOTO BENDI NA MSONDO NGOMA NANI ZAIDI?...KUONYESHANA KAZI JUKWAA MOJA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Kampuni ya Rainbow entertainment promotion iliyo chini ya mkurugenzi wake Hamisi Slim imeandaa show ya nguvu na ambayo haijapata kutokea kwa siku nyingi maeneo ya temeke pale watakapo zipambanisha bendi tatu katika jukwaa moja siku ya alhamisi ijayo tarehe 11/6/2015, bendi hizo ni G5 modern taarab, Yamoto bendi na Msondo ngoma baba ya muziki katika ukumbi wa Equator grill mtoni kwa azizi ally.


    Akizungumza na mtandao huu Slim alisema kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuwapa burudani wakazi wa wilaya ya temeke na vitongoji vyake kwani ni kipindi kirefu sana amekuwa akiombwa kuzipambanisha bendi hizo na sasa wakati ndio umefika, nawaomba wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi kwani pamoja na burudani lakini pia kutakuwa na ma-surprise kibao kutoka kwa bendi zote tatu.


   Show hiyo ambayo itaanza saa mbili kamili usiku hadi majogoo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu kumi tu za kitanzania 10,000/= kwa mtu mmoja na kwa ushauri tu ni vyema ukawahi nafasi mapema ili uweze kujionea burudani kwa umakini zaidi, ikumbukwe kwamba bendi yako ya G5 modern taarab ipo katika maandalizi ya kuingia kambini nje ya mkoa wa Dar baada tu ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuandaa vitu vipya na vya kisasa zaidi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni