Wakitokea katika ukoo ulio na damu ya muziki haswa, Vijukuu wa tego, Tarick tego na Khairat tego leo tarehe 27/6/2015 walikuwa wanamalizia shooting ya wimbo wao wa mama wa kambo ambao umekuwa gumzo kwa sasa afrika mashariki na kati, ndani ya maeneo yao ya kujidai temeke jiji Dar.
Katika shooting hiyo ambayo imejaa visa vya kweli na ambavyo vimekuwa vikitokea kila kukicha katika jamii yetu inayotuzunguka, watoto hao walifunika sana pale walipokuwa wakicheza style ya "min taarab" huku wapenzi na wadau waliopata bahati kuhudhulia shooting hiyo wakishangazwa na umahiri mkubwa wa watoto hao katika kuucheza na kuimba, zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo mtandao huu ulibahatika kuzipiga wakati wa uchukuaji wa video hiyo!.
TARICK TEGO NA KHAIRAT TEGO WAKISEREBUKA KATIKA SHOOTING HIYO!. |
KHAIRAT TEGO, HAPA AKIFOKEWA NA MAMA YAKE WA KAMBO HUKU AKIENDELEA KUOSHA VYOMBO!. |
KHARAT TEGO BAADA YAKUTESWA NA MAMA YAKE WA KAMBO, HAPO ANAKUTWA NA RAFIKI ZAKE WAKITOKEA SHULE. |
KHARAT TEGO AKIFAGILISHWA KINGUVU NA MAMA WA KAMBO WAKATI MUDA WA KUELEKEA SHULE UMEFIKA!. |
TARICK TEGO NA KHAIRAT TEGO WAKIPOZI KWA AJILI YA SHOOTING!. |
HAPA KHAIRAT TEGO AKICHEZA NDANI YA SHOOTING YA WIMBO HUO WA MAMA WA KAMBO!. |
KHAIRAT TEGO, BAADA YA KUTOROKA KWAO ALIKUJA KUKAA HAPA NDIPO ALIPOKUTWA NA RAFIKI ZAKE WAKITOKEA SHULE!. |
TARICK TEGO NA KHAIRAT TEGO WACHEZA KWA FURAHA KUBWA. |
TARICK TEGO AKISUBIRI DIRECTOR AMRUHUSU KUFANYA YAKE!. |
KHAIRAT TEGO AKIFAGILISHWA NA MAMA WA KAMBO HUKU AKIWA PEKU PEKU MIGUUNI. |
KHAIRAT TEGO AKIOSHA VYOMBO, HUKU RUNDO LA NGUO LIKIWA PEMBENI LIMSUBIRI KWA AJILI YA KUFUA. |
KHAIRAT TEGO AKIWA SEBULENI KWAO AKIANGALIA TELEVISHENI |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni