NA KAIS MUSSA KAIS.
Hatimae kile kitendawili cha nani atachaguliwa mshindi katika tuzo bora za kilimanjaro music awards 2014-2015 kimeteguliwa usiku wa jana pale katika ukumbi wa kisasa zaidi wa mlimani city jijini Dar es salaam.
![]() |
ISHA MASHAUZI, PICHA KWA HISANI YA SALUTI5. |
Bendi za Jahazi modern taarab na mashauzi morden taradance ziliendelea kuthibitisha ubora wao kama ilivyokuwa mwaka jana kwani zenyewe ndizo zilizofanikiwa kuchukuwa tuzo hizo kwa vipengele tofauti
![]() |
MFALME MZEE YUSUPH, PICHA KWA HISANI YA SALUTI5. |
Mambo mengi yalizungumzwa toka kwa wadau na mashabiki wa muziki huu kupitia vyombo mbalimbali vya habari hususani mitandao ya kijamii wakionekana kutoridhishwa na uteuzi uliofanywa na academy ya kili music award's kwa baadhi ya wasanii, lakini mwisho wa siku cha umuhimu ni ushindi tu, ndivyo ilivyotokea kwa bendi hizi mbili na kuzitupa mbali bendi zifuatazo Dar modern taarab, wakaliwao modern taradance, Ogopa kopa classic bendi na five star's modern taarab
![]() |
ISHA MASHAUZI AKIWA NA MENEJA WAKE SUMA LAGER, PICHA KWA HISANI YA SALUTI5. |
Katika tuzo hizo vioja vya hapa na pale havikukosa mfano ni pale mfalme mzee yusuph aliposhangazwa na Jina la Abdallah feresh mkurugenzi wa Dar taarab akionekana kutomtambua uwezo wake hususani utunzi wa mashairi, alihoji Feresh ni nai? kwanini nipambanishwe na yeye?labda ingekuwa watu kama Thabt Abdul, Hassan Ally na wengine lakini sio feresh alisema mzee yusuph.
Yafuatayo ni majina ya wasanii waliofanikiwa kujishindia zawadi
1.. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB
2.. MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI - ENRICO
3.. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB- MZEE YUSSUF
4.. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - MZEE YUSSUF
.5. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - ISHA MASHAUZI
6.. WIMBO BORA WA TAARAB (MAPENZI HAYANA DHAMANA)- ISHA MASHAUZI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni