TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 9 Juni 2015

UJIO MPYA WA WAKALI WA TOWN MODERN TAARAB, WAITIKISA NA KUIPA HOFU WAKALIWAO MODERN TARADANCE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Bendi mpya ya Wakali wa town modern taarab imeanzishwa hivi karibuni kijitonyama jijini  Dar chini ya mkurugenzi mkuu "Uncle Vam", bendi hii ambayo mpaka sasa inaundwa na waimbaji sita wakike na mmoja wakiume inatarajia kuingia kambini katika mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuandaa vibao vikali vipya.


MKURUGENZI WA WAKALI WA TOWN UNCLE VAM AKIWA NYUMBANI KWAKE.

    Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi huyo alisema, nimekuja kuleta ushindani wa kweli katika tasnia hii ya taarab hapa nchini, mimi si mgeni katika muziki huu wa taarab kwani wakati wa Five stars modern taarab ya Shark's the Don nilikuwepo na nazijua njia za uongozi wa taarab vizuri tu!. bendi yangu ina waimbaji chipukizi na wanaojua vyema kuimba, ing

awa kwa sasa nipo katika mazungumzo na waimbaji wenye majina makubwa takribani watatu ambao watajiunga na vijana hawa baada ya kufikia makubaliano yetu kimaslahi. Namba yangu ya simu mimi mkurugenzi ni 0712-311350 namba ingine ni 0716-447078 tuwasiliane kwa maoni na ushauri.


      Katika uchunguzi wa awali uliofanywa na mtandao huu kwa baadhi ya wadau wa taarab, wameonyesha kuanza kuihofia bendi hii kwani inaonekana kuja kuifunika bendi ya Wakaliwao modern taradance kulingana na majina yao kufanana kiasi na mfumo wa kuwa na waimbaji wachanga wenye uwezo. Kiukweli mimi ni mpenzi wa wakaliwao lakini hii bendi ya wakali wa town nadhani nia yao ni kuja kutuvuruga tu! kwanini wasitumie jina lingine? alimaliza kujieleza mama munirah!


    Mtandao huu unaendelea kufanya pilika pilka za kumtafuta mkurugenzi wa wakaliwao Thabit Abdul ili azungumzie ujio huu mpya wa bendi hii ambayo inafanana kiasi japo si sana na jina la bendi yake, tuendelee kusubiri wasomaji wangu wapenzi!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni