TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 13 Juni 2015

UMATI WAPAGAWA NA USIKU WA "TOROKA UJE" NA G5 MODERN TAARAB, YAMOTO BENDI SAMBAMBA NA MSONDO NGOMA!!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Siku ya alhamisi tarehe 11/6/2015 katika ukumbi wa Euqator grill mtoni kwa azizi ally jijini Dar kulikuwa na burudani ya nguvu toka katika bendi tatu jukwaa moja ambazo ni G5 modern taarab, Yamoto bendi na Msondo ngoma baba ya muziki


       Onyesho lilianza saa mbili kamili kwa msondo ngoma kupanda stejini na kuanza na ule muziki wa utangulizi, ilipofika saa tatu kamili ratiba ilianza kwa msondo hao hao kuendelea na burudani ya nyimbo zao kadhaa zilizotamba zamani na zinazoendelea kutamba sasa, hali iliyofanya umati mkubwa uliojitokeza katika onyesho hilo kuacha viti vyao na kuingia kati kucheza kwa pamoja, ilipotimu saa tano kamili zamu ya bendi ya G5 modern taarab iliwadia na vijana wakaingia kufanya yao.


YAMOTO BENDI

     Walianza kwa Ashura machupa kuimba wimbo wa "sina makuu" ambapo wadau walidata na kuanza kuingia kati kucheza na kumtunza pesa sana!, baadae aliingia sharobabu Ally star na wimbo wake uliotamba sana wa "Hawavumi lakini wamo", wapenzi walipiga kelele sana za mayowe kuonyesha ni kwa jinsi gani wanamkubali na wamekumbuka mbali sana, baadae alipanda Mwamvita shaibu na alipotoka yeye akaingia Khadija omary kopa na wimbo wake wa "Fahari ya mwanamke" ambao aliurekodi na G5 modern taarab, ilikuwa ni raha isiyo na kifani wadau na wapenzi walionekana kuchanganyikiwa kwa raha za malkia.


KHADIJA OMARY KOPA.

    Ndipo baadae akapanda Prince Muumin na wimbo wa "Kigodoro kimelowa maji" hapo ilikuwa mshikemshike kweli maana haijapata kutokea, inaonyesha kama wapenzi walikuwa wanamsubiri Muumin kwa jinsi walivyolipuka kwa shangwe ukumbi mzima ulilindima, ilidhihirika wazi kuwa Muumin bado wapenzi wana mkubari sana!, aliekuja kufunga dimba ni Fadhira mnoga kwa burudani tamu na ya kukata na shoka!.


ASHURA MACHUPA.

     Ilipofika saa saba na nusu usiku wakaingia Yamoto bendi ambapo walifanya yao mpaka saa tisa na nusu usiku, walipiga nyimbo zao zote zinazotamba sasa pamoja na baadhi mpya ambazo bado hazijapelekwa katika media, walisikika baadhi ya wapenzi waliofika wakisema ama kweli leo tume-enjoy sana maana kiu yote ya burudani imeisha ahsante sana Hamisi Slim mungu akupe maisha marefu, wewe ni mkombozi wa temeke yetu hususani maeneo yote ya mtoni.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni