TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 9 Julai 2015

AMIN SALMIN:- ABADANI SIWEZI KUWA MFUASI WA MZEE YUSUPH KWA KUTENGENEZA WIMBO WA DAKIKA SITA NDANI YA T MOTTO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Mkurugenzi wa T motto modern taarab Amin salmin ameuambia mtandao huu kuwa yeye si miongoni mwa watakaomfuata mfalme mzee yusuph kwa kutengeneza wimbo au nyimbo za dakika sita ndani ya bendi yake hiyo.


AMIN SALMIN MKURUGENZI WA T MOTTO MODERN TAARAB.

         Aliyasema hayo siku ya Ramadhan ishirini pale wadau wasanii na viongozi mbalimbali wa taarab nchini walipokuwa wamealikwa katika futari ya pamoja manzese jijini Dar nyumbani kwa mkurugenzi wa maja's modern taarab Hamisi majaliwa. Akizungumza kwa kujiamini Amin alisema kuwa haoni mantiki ya kutengeneza nyimbo ya dakika sita kama alivyofanya mfalme mzee yusuph katika wimbo wake mpya wa "kaning'ang'ania ng'ang'anu" na ule wa mkewe Leyla rashid "nina moyo sio jiwe" ambazo zote zina dakika za kushabihiana kidogo!.


      Unapoamua kutengeneza wimbo wa dakika sita basi elewa kisa au dhumuni la mtunzi halitotimia sababu taarab sio bongo fleva!, utalazimika kuyafanya maneno yawe machache kisha uwe una-rap zaidi ili kunogesha kama ambavyo amefanya yeye, ile sio taarab labda kama kuna jina lingine!, nimesikia kuna watu nao wameanza kuiga kutengeneza nyimbo zao kwa style hiyo. Naomba niwaambie kitu kimoja unapoamua kufanya jambo angalia na matokeo yake ya baadae na sio kuburuzwa tu eti sababu fulani kafanya huo sio usanii, mimi kamwe siwezi kuwa mfuasi wa mzee yusuph kwa kutengeneza nyimbo zenye style hiyo abadani.


WAIMBAJI WA T MOTTO MODERN TAARAB.

       Akimalizia Amin aliwaomba wapenzi wa bendi yake ya T motto kusubiri kitu cha "hakuna kuomba poo" kwani kwa sasa wapo jikoni kutengeneza na kwa taarifa tu wimbo huo hautokuwa na dakika sita bali utaimbwa kwa mapana na marefu na anaamini wapenzi watafurahi kwani Tmotto haijawahi kuwaangusha wapenzi wake daima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni