TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 9 Julai 2015

OMARY KISILA:- KUKOPI KATIKA TAARAB SIO TATIZO, ILA TATIZO KUBWA NI KUHAMISHA KILA KITU KAMA KILIVYO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

        Director anaefanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya muziki wa taarab hapa nchini tanzania Omary kisila amezungumzia suala linalopigiwa kelele sana na wadau wakiwalaumu waongozaji wa muziki huo yaani "ma-director" kwamba wamekuwa wakipoteza kabisa maudhui na ile radha ya muziki wa taarab kwa kuweka vipande vya nyimbo za dansi katika taarab.


OMARY KISILA DIRECTOR WA MUZIKI WA TAARAB NCHINI.

      Akizungumza na mtandao huu bora Kisila alisema si vibaya kukopi kipande fulani na kukitumia katika muziki unaoutengeneza ila kikubwa inatakiwa utumie akili ya ziada kukibadilisha kidogo ili kisiendane kabisa kama kilivyopigwa awali, tatizo letu sisi ma-director tumekuwa tukiamisha kipande kama kilivyo original yake na kukiweka katika taarab, hii kiukweli sio nzuri inaonekana kama sisi tumeshindwa kubuni cha kwetu na kuanza kuhamisha ili kujirahisishia.


OMARY KISILA.

      Nikitolea mfano hata wazee wetu wa zamani nao walikuwa wakikopi ila walikuwa wajanja sana, jaribu kusikiliza nyimbo za marehemu Juma bhalo, Issa matona, Malika na wengineo utagundua zile beat zao hadi uimbaji walikuwa wakikopi nyimbo za kihindi, kwahiyo sio dhambi kukopi wala haina shida ila kikubwa unakopi kwa style ipi? hapo ndipo palipo na changamoto kwetu sisi "ma-director" alimalizia kwa kusema!.


      Mtandao huu unawaahidi kwamba utafanya mahojiano na waongozaji wote wa muziki wa taarab ili kupata maoni yao juu ya suala hili lililozua mjadala mkubwa kwao, ni kwanini wamekuwa wakikopi sana vipande vya nyimbo za dansi na hata gospel nakuviingiza katika muziki wa taarab? je wameishiwa uwezo wa kubuni ama lah!, endelea kufuatilia ndani ya mtandao huu ili ufaidike...usikose!.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni