Muimbaji wa muziki wa dansi nchini Ramadhan masanja almaarufu Banza stone amefariki dunia leo saa saba na nusu mchana nyumbani kwao sinza jijini Dar.
BANZA STONE ENZI ZA UHAI WAKE.
Kaka wa marehemu ndugu Hamisi masanja aliuthibitishia mtandao huu kuwa ndugu yake ni kweli amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu sana, unajua hali ya ndugu yangu ilianza kubadilika tangia jana alikata kauli kabisa jambo lililotufanya wana ndugu kutaharuki.
Taarifa za utaratibu wa mazishi tutawaletea kupitia kwenye mtandao huu huu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Ikumbukwe marehemu Banza stone aliwahi kutamba na nyimbo kama Elimu ya mjinga, Aungurumapo simba na hata kwa upande wa taarab aliwahi kuimba wimbo uitwao kuzaliwa mjini ambao alitungiwa na thabit abdul mkombozi mkurugenzi wa wakaliwao modern taarab.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni