TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 17 Julai 2015

RAIS BARRACK OBAMA AAHIRISHA SHOW YA OGOPA KOPA CLASSIC BENDI NAIROBI KENYA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Ile show ya nguvu toka kwa ogopa kopa classic bendi iliyokuwa ifanyike nairobi nchini kenya tarehe 24/7/2015 imeahirishwa kutokana na ujio wa Rais Barrack Obama wa marekani katika nchi hiyo ya kenya!.


SHOW YA NAIROBI YAAHIRISHWA!.

         Show hiyo ambayo ilikuwa ifanyike katika ukumbi wa Nairobi city hall imeahirishwa kutokana na hali ya kiusalama zaidi, akizungumza na mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com mtoto wa malkia khadija kopa aitwae black kopa alisema show imeahirishwa kwa kuwa rais obama anatarajiwa kudhuru nchini kenya siku ya tarehe 24/7/2015 siku ambayo wao ogopa kopa ndio ilikuwa wafanye onyesho lao pale Nairobi city hall,


       Uongozi wa ogopa kopa unawaomba radhi wapenzi wake wa Nairobi kwa dharura hiyo kwani hawatoweza kufanya onyesho kama ilivyo tarajiwa!. kiukweli tatizo hilo lipo nje ya uwezo wetu na lazima taratibu za nchi husika zifuatwe ili kulinda usalama na maadili ya nchi, kikubwa tunawaomba wawe wavumilivu kwani tutakwenda tena nairobi panapo majaaliwa alimaliza kusema.


SHOW YA MOMBASA IPO KAMA KAWAIDA!.

     Wakati huo huo ile show ya tarehe 25/7/2015 ambayo imepangwa kufanyika mombasa municipal stadium itafanyika kama kawaida na uongozi wa ogopa kopa umewaomba wakazi wa maeneo hayo na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kwani malkia amewaandalia kitu maalum kabisa kwa ajili yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni