Mkurugenzi wa G5 modern taarab Hamisi slim hatimae leo amefanikiwa kuchukuwa fomu ya kugombea udiwani wa kata mtoni kupitia chama cha C.C.M.akisindikizwa na wapambe kibao Hamisi slim alifika katika ofisi za C.C.M kata ya mtoni na kupokewa na uongozi wa chama hicho na kupelekwa moja kwa moja kukabidhiwa fomu hizo.
Huku nje walionekana watu wengi wakishangilia na kulitaja jina la Hamisi slim kuwa ndio chaguo lao na wanaamini kama atafanikiwa kuwa Diwani wao atawaletea maendeleo makubwa sana, katika tukio la kushangaza na kustaajabisha alisikika mmasai mmoja akizungumza kuwa huyu Slim ndio kikwete wa eneo letu la mtoni sisi masai tunampenda sana!, walipitisha harambee ya pesa pale pale ili kumpa Hamisi slim kama chachu ya kumtia moyo na hamasa ya kuendelea na kampeni zake za kugombea nafasi ya udiwani kwa tiketi ya chama cha C.C.M.
Zifuatazo ni picha "11" za matukio akikabidhiwa fomu rasmi:-
MKURUGENZI WA G5 MODERN TAARAB HAMISI SLIM AKISAINI OFISI ZA CCM MTONI. |
HAMISI SLIM AKIONYESHA FOMU YAKE KWA WANANCHI BAADA YA KUKABIDHIWA. |
MYINYIJUMA MUUMIN AKIWA NA WADAU KADHAA WAKIMSUBIRI MUHESHIMIWA. |
WADAU WAKIWA WAMELIZUNGUKA GARI JIPYA KABISA LA MUHESHIMIWA SLIM. |
MUHESHIMIWA HAMISI SLIM AKIJADILI JAMBO NA BAADHI YA VIONGOZI WA CCM. |
MUHESHIMIWA HAMISI SLIM, HAPA AKIKABIDHIWA FOMU YA KUGOMBEA UDIWANI. |
HAMISI SLIM AKIWA NA WATU WAKE WA KARIBU WAKIIONYESHA FOMU KWA WAANDISHI WA HABARI. |
MUHESHIMIWA HAMISI SLIM AKIWA NJE YA OFISI ZACHAMA. |
HAPA AKIJIANDAA KUONDOKA ENEO LA OFISI ZA CHAMA CHA CCM. |
ILIKUWA FURAHA HADI KWA MASAI. |
RAIA WAKIONYESHA USHIRIKIANO KWA KUMCHANGIA PESA MUHESHIMIWA HAMISI SLIM. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni